KATIKA KUIMARISHA BENCHI LA UFUNDI KLABU YA COASTAL UNION YA TANGA,UMEINGIA MKATABA WA MWAKA MMOJA NA ALIYEKUWA KOCHA WA MAKIPA WA YANGA,MFAUME ATHUMANI SAMATA ##

Akizungumza leo ,Ofisa Habari wa Coastal Unioon  amesema kuwa kocha huyo anachukua mikoba ya Razack Siwa aliyewahi kuwanoa makipa wa  timu hiyo kabla ya kuondoka.

Assenga amesema kuwa kocha huyo aliwahi kuzifundisha timu za soka Yanga ,Ashanti United na Timu ya Taifa ya Vijana U-20 wana matumaini makubwa sana ataimarisha safu ya walinda milango kwenye kikosi hicho ili kuweza kukipa mafanikio.

Akizungumzia mipango yake mara baada ya kutua kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyokuwa yakiendelea jana kwenye viwanja wa Disuza jijini Tanga,Kocha Mfaume alisema kuwa malengo yake makubwa ni kuhakikisha kikosi cha timu hiyo kinashika nafasi za juu kwenye michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara.

Kocha huyo ndio aliyeiongoza timu ya Yanga kufungwa goli saba mpaka ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ilipomalizika akiwanoa makipa kama vile Mustapha Barthezi na Yaw Berko.
Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment