MTANI JEMBE YA 2014 SIMBA KAMALIZA MWAKA VIZURI GOLI MBILI TU ZIMETOSHA NA MILIONI ZAO TENA ACHA KABISA ##

SIMBA SC imeendeleza ubabe wake kwa mahasimu wao, Yanga SC katika  mechi za Nani Mtani Jembe, baada ya jioni hii kuichapa mabao 2-0  Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Desemba mwaka jana, Simba iliichapa Yanga SC



mabao 3-1 katika  mechi ya Mtani Jembe, inayoandaliwa na wadhamini wa timu hizo,  Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro. 

Katika mchezo wa leo, hadi mapumziko, Simba SC ilikuwa tayari  inaongoza kwa mabao hayo mawili, yaliyotiwa kimiani na kiungo  Awadh Juma na mshambuliaji Elias Maguri.
Awadh Juma alifunga bao la kwanza baada ya kuanzishiwa mpira wa  adhabu uliopigwa na Emmanuel Okwi dakika ya 30, umbali wa mita 23.

Elias Maguri aliifungia Simba SC bao la pili dakika ya 42 akimalizia mpira uliorudi baada ya kugonga mwamba kufuatia shuti  la Mganda, Simon Sserunkuma.

Kiungo wa Yanga SC, Mnyarwanda Mbuyu Twite aliumia dakika ya 39 na  kutoka nje, nafasi yake ikichukuliwa na Hassan Dilunga. 

Mshambuliaji mpya Yanga SC, Mliberia Kpah Sherman alionyesha ni  machachari, lakini hakupata ushirikiano mzuri pale mbele.
Refa Jonesia Rukyaa kutoka Bukoba mkoani Kagera, pamoja na kwamba  ni mwanamke, lakini alijitahidi kuumudu mchezo huo kadiri ya uwezo  wake. 

Mashabiki wa Yanga SC walianza kuondoka uwanjani mapema tu baada  ya bao pili, huku wengine wakivamia chumba cha kubadilishia nguo  wachezaji.

Kipindi cha pili, kocha wa Simba SC, Mzambia Patrick Phiri alianza  na mabadiliko, akimuingiza Nahodha Joseph Owino kwenda kuchukua  nafasi ya Juuko Murushid, wakati kocha Mbrazil wa Yanga SC, alimuingiza Salum Telela kwenda kuchukua nafasi ya Emerson na  Danny Mrwanda kumrithi Andrey Coutinho.

Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Ivo Mapunda, Nassor Masoud ‘Chollo’,  Mohammed Hussein ‘Tshabalala’/Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ dk66,Hassan Isihaka, Juuko Murushid/Joseph Owino dk47, Jonas Mkude,  Ramadhani Singano ‘Messi’/Said Ndemla dk74, Awadh Juma, Elias  
Maguri/Dan Sserunkuma dk84, Simon Sserunkuma/Shaaban Kisiga  ‘Malone’ dk84 na Emmanuel Okwi.

Yanga SC; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul/Hussein Javu dk79,  Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mbuyu  Twite/Hassan Dilunga dk39, Emerson Roque/Salum Telela dk55, Haruna  Niyonzima, Kpah Sherman/Mrisho Ngassa dk63, Simon Msuva na Andrey  Coutinho/Danny Mrwanda dk46.
Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment