Mheshimiwa Ummy Mwalimu (Mb) Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais alifanya ziara ya kukagua Mazingira Mkoani Mtwara hususani katika eneo la Mdenga, Manispaa ya Mtwara.
Chimbuko la ziara hii ni malalamiko yaliyotolewa na wananchi kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Abdulrahman Kinana alipokuwa kwenye ziara ya kikazi mkoani humo
Afisa Uhusiano wa kampuni ya SBS, Bw. Geofrey
Kanenge (katikati) akitoa
maelezo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu (Mb)
(wa pili kushoto) kuhusu udhibiti wa
utiririshaji wa maji taka yatokanayo na usafishaji wa mapipa yenye kemikali
unavyofanywa na kampuni hiyo wakati wa ziara ya ukaguzi wa mazingira mkoani
Mtwara.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa
Ummy Mwalimu (katikati) akipata maelezo kuhusu ubanguaji wa korosho kutoka kwa
Uongozi wa Kiwanda cha Micronix kilichopo mkoani Mtwara wakati wa ziara aliyoifanya mkoani humo.
Sehemu ya Wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri
Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu (hayupo pichani) wakati wa
ziara ya kukagua hali ya Mazingira ya viwanda aliyoifanya mkoani Mtwara
Eneo la bwawa la asili la Mdenga lililofukiwa
kinyume cha sheria na kampuni ya SBS inayojishughulisha na urejelezaji wa taka
mkoani Mtwara na kusababisha uharibifu wa mazingira katika eneo hilo.
0 comments:
Post a Comment