Kamati ya
Uendeshaji na Usimamizi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imethibitisha
ushindi wa pointi na mabao matatu kwa timu za Majimaji na Toto Africans baada
ya mechi zao za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kuvurugika kutokana na sababu
mbalimbali.

Toto Africans imepewa ushindi huo kwa mujibu wa Kanuni ya 41(3) ya FDL baada ya vurugu za washabiki wa Geita Gold kusababisha mechi hiyo iliyochezwa Februari 10 mwaka huu kwenye Uwanja wa Nyankumbu mkoani Geita kuvunjika dakika ya 12.
Pia
Kamati hiyo iliyokutana Dar es Salaam jana (Februari 12 mwaka huu) imezuia
mechi za FDL kuchezwa kwenye uwanja huo ambao hauna uzio wa kutenganisha
wachezaji na washabiki kwa sababu za kiusalama.
Naye
mchezaji Venance Joseph wa Geita Gold ambaye alimpiga kichwa refa akipinga
adhabu ya penalti iliyotolewa dhidi ya timu yake kwenye mechi hiyo
amesimamishwa wakati akisubiri kosa lake kusikilizwa na Kamati ya Nidhamu ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Malalamiko
ya Friends Rangers kwenye mechi dhidi ya Majimaji yametupwa na kupigwa faini ya
sh. 500,000 kwa kusababisha mchezo huo uliochezwa Januari 29 mwaka huu Uwanja
wa Majimaji mjini Songea kuvunjika dakika ya 39. Adhabu hiyo imetolewa kwa
kuzingatia Kanuni ya 28(4) ya FDL.
Friends
Rangers imepoteza mechi hiyo kwa mujibu wa Kanuni ya 28(1) ya FDL, Majimaji
kama ilivyo Toto Africans imepewa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu.
Naye
Kocha wa Friends Rangers, Herry Chibakasa (Mzozo) suala lake limepelekwa kwenye
Kamati ya Nidhamu ya TFF ili aweze kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa
Kanuni ya 39(8) ya FDL kwa kuhamamisha vurugu kwenye mechi dhidi ya Majimaji.
Mwamuzi
John Mafuru wa Mbeya aliyechezesha mechi ya Majimaji na Friends Rangers
amefungiwa miezi 12 (kumi na mbili) kwa kutozingatia sheria kiasi cha kuvuruga
mchezo. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 37(1) ya FDL.
Pia
Kamishna wa mechi hiyo Kim Rajab wa Dodoma amefungiwa miezi 12 (kumi na mbili)
kwa mujibu wa Kanuni ya 38(1) ya FDL kwa kutoa taarifa zisizo sahihi.
Lipuli
ya Iringa imepewa ushindi wa mabao matatu na pointi tatu baada ya timu ya KMC
(Tessema) kumchezesha mchezaji Morris Paulo Katumbo aliyekuwa na kadi tatu za
njano kinyume na Kanuni ya 41(12) ya FDL. Katumbo ambaye alipata kadi hizo
kwenye mechi namba 85, 100 na 112 alicheza mchezo huo uliomalizika kwa timu ya
KMC kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
0 comments:
Post a Comment