FIFA Leo hii imetoa Listi ya Ubora Duniani na zile Nchi 5 Bora, zikiongozwa na Mabingwa wa Dunia Germany ziko Nafasi zao zile zile huku Tanzania ikiporomoka Nafasi 3 na kushika Nafasi ya 107.
Kwa Afrika, Nchi ya juu kabisa bado ni Algeria ambayo iko Nafasi ya 18 wakifuatiwa na Mabingwa Wapya wa Afrika, Ivory Coast, ambao wako Nafasi ya 20, wakati Ghana, waliofungwa na Ivory Coast kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, wameruka Nafasi 12 na sasa wapo Nafasi ya 25.
Wenyeji wa AFCON 2015, Equatorial Guinea, wamepaa Nafasi 69 na kukamata Nafasi ya 49 pamoja na Congo.
Listi ya Ubora Duniani inayofuata itatolewa Machi 12.
10 BORA:
1. Germany
2. Argentina
3. Colombia
4. Belgium
5. Netherlands
6. Brazil
7. Portugal
8. France
9. Uruguay
10. Spain
0 comments:
Post a Comment