
Chidi alipandishwa kizimbani mahakamani hapo kusomewa mashtaka matatu ya
kukutwa na madawa ya kulevya mwaka jana.
Alikuwa nje kwa dhamana ya shilingi milioni 1 pamoja na wadhamini wawili
wasiokuwa na hatia. Faini anayotakiwa kulipa ni shilingi laki tisa.
Tukio hilo lilitokea October 25 mwaka jana katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa anaelekea jijini Mbeya
kwenye show.
Hata hivyo, mwimbaji huyo wa wimbo Dar es Salaam Stand Up, ameachiwa huru baada ya kulipa faini hiyo ya Sh. 900,000
na amerejea nyumbani kwao Ilala kuendelea na maisha ya uraiani.
0 comments:
Post a Comment