Chama cha
kandanda mkoa wa Dar es salaam DRFA,kimewapongeza wawakilishi wa Tanzania bara katika michuano
ya vilabu barani afrika klabu ya Azam FC
na Yanga SC,kwa kuanza na ushindi katika
mechi zao za mkondo wa kwanza mwishoni mwa juma.
Yanga
walikuwa wa kwanza kuwapa raha watanzania siku ya jumamosi katika uwanjwa wa taifa jijini,baada ya
kuifunga mabao 2-0 timu ya maafande wa
Polisi toka Botswana BDF 11,mabao yete hayo yakitupiwa nyavuni na mshambuliaji
Amis Tambwe,ikiwa ni mchezo wa kuwania kombe
la shirikisho.
Kwa upande
wa Azam FC,wao waliwafunga wababe wa soka huko Sudan klabu ya El-Merekh kwa mabao 2-0 yaliyofungwa
na Didier Kavumbagu pamoja na John
Rafael Bocco,katika mchezo wa kuwania kombe la
klabu bingwa
uliopigwa katika dimba la Azam Cpmplex Chamazi.
Mwenyekiti
wa DRFA,Almas Kasongo,amewapongeza wawakilishi hao wa Tanzania kwa hatua hiyo
nzuri waliyoanza nayo,na kusema kuwa
maandalizi
yaliyofanywa na vilabu hivyo kuelekea mashindano hayo
ya afrika,pamoja na ubora wa wachezaji na
makocha,ni dhahiri kwamba vitafanikiwa kuvuka katika hatua hiyo ya kwanza.
Kasongo,pia
amesema DRFA imeridhishwa na muitikio wa mashabiki wa
Dar es
salaam na maeneo mengine nje ya jiji kwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia mechi
hizo mbili,na kuwapongeza pia viongozi wa vilabu kwa matayarisho waliyoyafanya
licha ya dosari ndogo ndogo zilizojitokeza.
MICHUANO YA
LIGI YA MKOA DAR INAENDELEA.
Michuano ya
ligi ya mkoa wa Dar es salaam inaendelea tena wiki hii
kwa timu 8 kushuka katika viwanja tofauti,kupambana
ili kuusaka
ubingwa huo
pamoja na kupata nafasi ya kuingia katika ligi daraja
la pili taifa.
Mechi za leo
Februari 16,2015/Azania Ngano watakipiga dhidi ya Yanga U20 (Katika uwanja wa Karume),Stakishari
watacheza na FFU (uwanja wa
B.Mkapa),Changanyikeni wataumana dhidi ya Tuamoyo (uwanja wa MWL/Nyerere) na New Kunduchi
wataoneshana kazi dhidi ya Sinza Stars
(uwanja wa Kines).
Kivumbi
hicho kitaendelea tena kesho Kutwa Februari 18,2015 kwa
Simba U20
kucheza na Ukonga UTD (Uwanja wa karume),Red Coast watacheza dhidi ya Shababi
(MWL/Nyerere),Zakhem watacheza na Sifa UTD
( Uwanja wa Bandari) na Beirahotspurs watakipiga dhidi ya Pan
African (uwanja wa Kines).
IMETOLEWA NA DRFA
Mkuu wa
Kitengo cha Habari na Mawasiliano DRFA
0 comments:
Post a Comment