Timu ya Taifa ya Tanzania ya Mpira wa Miguu wa
Ufukweni (Beach Soccer) jana imeibuka na
ushindi wa mabao 5- 3 ugenini dhidi wa wenyeji timu ya Taifa ya Kenya kwenye
mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa
fukwe za Hotel ya Big Tree Pirates jijini Mombasa.
Katika mchezo huo mabao ya Tanzania yalifungwa na Ali Rabbi mabao manne na Mwalimu Akida bao moja .
Kipindi cha
kwanza kilimazika kwa Tanzania kupata mabao 2 Kenya 1, kipindi cha pili kilimalizika Tanzania 4 Kenya
3 na kipindi cha tatu na cha mwishokwa
mchezo kimalizika kwa Tanzania kupata mabao
5 Kenya 3.
Mechi ya
marudiano inatarajiwa kuchezwa jumamosi wiki hii Februari 21, 2015 jijini Dar es salaam, na endapo timu
ya Taifa ya Tanzania itafanikiwa kuwatoa
Kenya, itacheza na timu ya Taifa ya Misri katika hatua inayofuata.
Mchezo wa
kwanza utafanyika kati ya tarehe 7,8 Machi 2015 jiji Dar es salaam na marudiano yatafanyika nchini
Misri kati ya tarehe 13,14 Machi 2015.
Timu inarejea leo jijini Dar es salaam majira
ya saa 11 jioni ikitokea jijini Mombasa
nchini Kenya.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU
TANZANIA (TFF)
0 comments:
Post a Comment