Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe Zitto Zuberi Kabwe (pichani) usiku
huu ametangaza rasmi Bungeni Dodoma kuachia kiti hicho alichokipata kupitia
CHADEMA.
Mhe. Kabwe ametangaza kung'atuka nafasi hiyo baada ya Mwenyekiti
wa Bunge Mhe Mussa Hassan Zungu Kumruhusu kutoa kauli binafsi mara baada ya
wabunge kumaliza kupitia vifungu vya sheria ya Maafa ambayo hata hivyo
haikupitishwa kwa kutotimia akidi ya wabunge ambao nusu yao hawakuwepo
ukumbini.
Juu Mheshimiwa Zitto Kabwe na wabunge wengine wakitoka
Bungeni mjini Dodoma leo. Chini akiwa na Mbunge wa Ludewa Mhe. Deo Filikunjombe
(kuhoto) na Mbunge mwingine
Mhe Zungu alimtakia kila la heri Mbunge huyo machachari ambaye
amesema ameamua kuachia ngazi baada ya chama chake kumfukuza. Hata hivyo
alimalizia kwa kusema kwamba Mungu akipenda atakuwa nao tena mwezi
Novemba mwaka huu. Hakufafanua. Video ya tamko lake hilo hii hapa...
Mhe.Zitto Kabwe akiongea na waandishi wa
Habari usiku huu mara baada ya Kuwaaga Wabunge Baada ya kuwasomea barua
aliyomwandikia Mhe.Spika ya Kung'atuka Ubunge baada ya kuvuliwa Uanachama na
chama chake cha CHADEMA
|
0 comments:
Post a Comment