Mkuu
wa Mkoa wa Tanga Mhe. Magalula S. Magalula akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Ofisini kwake
Kaimu
Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bw. Ramadhani Kaswa
(Kushoto ) na baadhi ya Waandishi wakati wa mkutano
Baadhi
ya Waandishi wa Habari wakati wa mkutano
Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Tanga kwa niaba ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na
Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama Tanzania inapenda kuwatangazia
Wananchi kuwa Mkoa wa Tanga unatarajia
kuwa mwenyeji wa maadhimisho ya Siku ya Utepe Mweupe Kitaifa itakayofanyika
Machi 15, Mwaka huu.
Siku ya
Utepe Mweupe ni mwendelezo wa juhudi za Serikali katika kupunguza na kutokomeza kabisa vifo vya akina mama na
watoto wachanga.Maadhimisho haya ambayo hufanyika Machi 15 kila mwaka yana lengo la kuwakumbuka
na kuwaenzi wanawake waliopoteza maisha kutokana na matatizo ya uzazi.
Siku hii pia
hutumika kujadili mikakati ya kuzuia vifo vingine visitokee. Kauli mbiu ya
mwaka huu ni “WAJIBIKA MAMA NA MTOTO MCHANGA AISHI”. Kauli mbiu hii inalenga kuhamasisha
uwajibikaji wa kila mmoja wetu kuanzia mama mjamzito nwenyewe na familia
yake, jamii na uongozi katika
kuhakikisha kuwa hakuna mama wala mtoto mchanga anayepoteza maisha kutokana na
sababau ambazo zingeweza kuzuilika.
Aidha,
kutakuwepo na shughuli mbalimbali ambazo zitaambatana na maadhimisho haya
katika wiki ya kuelekea siku yenyewe ambazo ni pamoja na uchangiaji damu
salama, kushiriki katika zoezi la sauti ya jamii,kushiriki katika matembezi ya
mshikamano na mkutano siku ya kilele.
Asilimia 75 ya vifo vingi nchini vinatokana na
kutoka damu kwa wingi, maambukizi, shinikizo la damu na utoaji mimba. Wanawake
24 wanafariki kila siku na wengine hupata ulemavu wa kudumu.
Serikali kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali imeendelea kuweka mikakati madhubuti ili
kupunguza vifo vya mama na mtoto. Kwanza imeelekeza nguvu zake katika kutoa
elimu ya uzazi salama na pia imeelekeza Halmashauri zote Mkoani kuwa na
kipengele mahususi cha bajeti kinacholenga kuhakikisha kuwa huduma za dharura
za uzazi zinapatikana karibu na akina mama na watoto.
Kutokana na
juhudi za serikali na wadau mbalimbali, matunda yameshaanza kuonekana miongoni
mwetu. Kwa mfano katika Mkoa wa Tanga vifo vya mama na mtoto vimepungua kutoka
idadi ya akina mama 101 kati ya wakina mama 45,256 waliojifungua kwa mwaka 2013
hadi kufikia idadi ya akinamama 69 kati ya wakina mama 47,692 waliojifungua kwa
mwaka 2014 na idadi ya watoto 429 kati ya watoto 44,852 waliozaliwa kwa mwaka 2013. Serikali inaendelea na mapambano kuhakikisha
afya ya mama na mtoto iko salama.
Kupunguza
vifo vya mama na mtoto vinavyotokana na matatizo wakati wa kujifungua ni moja ya malengo 8 ya Milenia. Hili ni lengo
namba tano ambalo linalenga kupunguza vifo vya akina mama vinavyoyokana na
matatizo wakati wa kujifungua kwa asilimia sabini na tano (75%) ifikapo mwaka
2015.
Nawashukuru
na kuwapongeza wenzetu wa Utepe Mweupe na wadau wengine kwa kujikita katika
kampeni ya uhamasishaji ili kupunguza na kutokomeza vifo vya mama na mtoto.
Napenda
kutoa wito kwa wananchi kuhakikisha kuwa kila mmoja anatekeleza wajibu wake ili
kuokoa maisha ya mama na mtoto. Pia naviomba vyombo vya habari kuungana na
makundi mengine katika jamii kuwa sauti ya akina mama ili kupunguza vifo vya
mama na mtoto.
Kwa pamoja
tunaweza kuzuia vifo vya mama na watoto wachanga
“Wajibika
Mama na Mtoto Mchanga Waishi”
0 comments:
Post a Comment