Wanaume
katika eneo la Meru mashariki mwa Kenya ambao hawana uwezo wa
kuwatosheleza wake zao kupitia tendo la ngono sasa wametakiwa kutokuwa
na wasiwasi.
Mwakilishi wa wanawake katika eneo hilo Florence
kajuju ameanza mpango wa kuwahamasisha wanaume kutumia miraa badala ya
ya pombe haramu .
Akizungumza na gazeti la The Nairobian nchini
Kenya,kiongozi huyo amesema kuwa pombe haramu hushusha nguvu za kiume na
kuwafanya wanaume kushindwa kuwatosheleza wake zao.
''Ni pombe kama hizi ambazo huathiri nguvu za kiume na kusababisha utasa miongoni mwa wanaume'',alisema.
Kajuju
ambaye anasema anapenda miraa aliudhika alipogundua kwamba eneo la Meru
ni miongoni mwa maeneo ambayo wanaume hawana uwezo wa kutafuta watoto
.
''Vijana wetu wameathirika vibaya na pombe haramu na lazima tuwaokoe''.
Alisema kuwa wale waliopiga marufuku uuzaji wa miraa katika mataifa yao wanafaa kugundua umuhimu wa zao hilo miongoni mwa jamii.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment