Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda
akionyesha kitabu kinachoeleza Maendeleo na historia ya Takwimu katika
Bara la Afrika alichokizindua leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Rais
wa Taasisi ya Kimataifa ya Takwimu (ISI) Bw. Vijay Nair na kulia ni
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda
akizindua kitabu kinachoeleza Maendeleo na historia ya Takwimu katika
Bara la Afrika alichokizindua leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Rais
wa Taasisi ya Kimataifa ya Takwimu (ISI) Bw. Vijay Nair na Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kushoto kwa Waziri Mkuu na Prof.
Ben Kiregyeza (kulia) ambaye ndiye mwandishi wa kitabu hicho.
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda
akifungua Kongamano la Kimataifa la Siku 3 la Wakuu wa Taasisi za
Takwimu wa nchi 38 za Afrika na 18 kutoka nje ya Bara la Afrika leo
jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa
ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa awali akizungumza na Wakuu wa Taasisi za
Takwimu wa nchi 38 za Afrika na 18 kutoka nje ya Bara la Afrika
waliohudhuria Kongamano la Siku 3 la Kimataifa kujadili Matumizi ya
Takwimu leo jijini Dar es salaam.
Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya
Takwimu (ISI) Bw. Vijay Nair akizungumza kabla ya uzinduzi wa Kongamano
la Kimataifa la masuala ya Takwimu la Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa
kutoka Afrika na nje ya Afrika.
Waziri Mkuu akizungumza jambo na
Makamu wa Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Takwimu (ISI) Bi. Irena
Krizman leo jijini Dar es salaam mara baada ya kufungua kongamano la
Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi 38 za Afrika na 18 kutoka nje ya
Bara la Afrika. Katikati ni mjumbe kutoka ya Kusini Bw. Pali Lihohla.
Waziri Mkuu akizungumza
akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam mara baada
ya kufungua kongamano la Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi 32 za
Afrika na 18 kutoka nje ya Bara la Afrika.
Waziri Mkuu akizungumza jambo na
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu mara baada ya kufungua
kongamano la Kimataifa la Wakuu wa Taasisi za Takwimu kutoka nchi 32 za
Afrika na 18 za nje ya Bara la Afrika.
Waziri Mkuu akizungumza akiwa
katika picha ya pamoja na Wakuu wa Taasisi za Takwimu kutoka nchi 32 za
Afrika na 18 za nje ya Bara la Afrika waliohudhuria Mkutano wa siku 3
wa Takwimu jijini Dar es salaam.
……………………………………………………..
Habari Picha- na Aron Msigwa/MAELEZO.
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda
amesema kuwa Serikali itaendelea kutoa kipaumbele katika matumizi ya
takwimu sahihi na kuweka mifumo mizuri ya kuwarahisishia wananchi na
taasisi mbalimbali kupata takwimu za masuala mbalimbali kutoka
Serikalini ili ili waweze kupanga mpango ya maendeleo.
Akifungua Kongamano la Kimataifa
la Siku 3 la Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi 38 za Afrika na 18
kutoka nje ya Bara la Afrika leo jijini Dar es salaam Mhe. Pinda amesema
kuwa nchi za Bara la Afrika ili ziweze kuwa na maendeleo endelevu
yanayotafsiriwa lazima zitoe kipaumbele katika matumizi ya Takwimu
sahihi.
Amesema Tanzania ni miongoni mwa
nchi za Bara la Afrika zilizopiga hatua kubwa katika kuweka mifumo ya
kurahisisha upatikanaji wa takwimu za masuala mbalimbali yakiwemo ya
Idadi ya watu, takwimu za masuala ya Afya na masuala mbalimbali
yanayohusu shughuli mbalimbali za uchumi wa Kaya binafsi.
“ Mpango wowote ambao hautumii
takwimu sahihi hauwezi kuzaa matunda, Lengo letu Serikali ni
kuhakikisha kwamba tunakuwa na takwimu sahihi kuhusu idadi ya wananchi
wetu, sekta ya afya, Elimu, Biashara, Kilimo na mifugo yetu ili tuweze
kutatua changamoto mbalimbali zinazotukabili” Amesisitiza.
Ameeleza kuwa upatikanaji wa
Takwimu sahihi katika Bara la Afrika hususani nchini Tanzania katika
masuala ya Kilimo, Chakula na Mifugo kutasaidia kutatua changamoto
mbalimbali zinazowakabili wakulima na wafugaji na kuwawezesha
kupunguza idadi ya mifugo waliyonayo kwa kuwa na ufugaji wenye manufaa
na endelevu.
Ametoa wito kwa nchi za Afrika
kuendelea kujenga taasisi imara za Takwimu na kuongeza bajeti za
kugharamia uwekaji wa mifumo rafiki ya upataji wa takwimu za masuala
mbalimbali ili kuwawezesha wananchi kupata takwimu bila vikwazo na
kuweka wazi kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kuijengea uwezo Ofisi
ya Taifa ya Takwimu (NBS) ili iweze kutekeleza kikamilifu majukumu yake.
Aidha, ameitaka Ofisi ya Taifa ya
Takwimu kutoa takwimu rahisi zinazoeleweka na kundi kubwa la watumiaji
ametoa na kutoa wito kwa wadau mbalimbali kutoka sekta ya Umma na
Binafsi, viongozi na wanasiasa kujenga utamaduni wa kutumia takwimu
kutoka vyanzo sahihi ili taasisi wanazoziongoza ziwe imara na zenye
matokeo.
Kwa upande wake Rais wa Taasisi ya
Kimataifa ya Takwimu (ISI) Bw. Vijay Nair akizungumza kabla ya uzinduzi
wa Kongamano hilo la Kimataifa amesema kuwa ili kujenga jamii Imara
yenye Ubunifu na inayolenga kupata mabadiliko lazima matumizi ya takwimu
sahihi yazingatiwe.
Amesema kuwa Taasisi anayoiongoza
ya ISI imekuwa mstari wa mbele katika kuhimiza matumizi ya Takwimu
sahihi, kujenga taasisi imara zenye wataalam wenye weledi katika masuala
ya Takwimu katika nchi mbalimbali za Afrika.
Ameeleza kuwa taasisi yake imekuwa
ikifanya kazi ya kuendesha Warsha na Makongamano katika nchi mbalimbali
duniani hasa zile zinazungumza lugha ya Kiingereza na Kifaransa kwa
kuwakutanisha wakuu wa taasisi na viongozi wengine wakuu wa ngazi ya
mawaziri ambao hukutana kujadili na kubadilishana uzoefu kuhusu umuhimu
wa matumizi ya takwimu kwa maendeleo ya nchi zao.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa
ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa awali akizungumza kabla ya kumkaribisha
mgeni rasmi kufungua Kongamano hilo la Kimataifa amesema kuwa Tanzania
inaendelea kufanya vizuri katika kuimarisha uwazi katika matumizi ya
Takwimu sahihi.
Amesema kuwa licha ya kuwepo kwa
tafsiri tofauti ya neon masikini kati ya nchi moja na nyingine, Ofisi
ya Taifa ya Takwimu inaendelea kuhuisha takwimu mbalimbali ili ziweze
kuakisi na kukidhi mahitaji ya sasa ya matumizi ya wadau mbalimbali
kitaifa na Kimataifa.
“Sisi kama Ofisi ya Taifa ya
Takwimu nchini Tanzania tunaendelea kuimarisha shughuli zetu ili
kuendelea kujenga uchumi imara kwa takwimu sahihi, tumeendelea kutoa na
kubainisha viashiria vya ukuaji wa uchumi wetu kwa ngazi ya taifa,
kutoa takwimu za Sensa ya Watu na Makazi pamoja na taarifa za Sekta
mbalimbali nchini” Amesema.
0 comments:
Post a Comment