YANGA MABINGWA MSIMU WA 2014 -2015 KWA MARA 25 WANALIBEBA TAJI ##

Yanga hii leo wametwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Vodacom kwa Msimu wa 2014/15 baada ya kuichapa Polisi Moro Bao 4-1 katika Mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Ushindi huu umewafikisha Pointi 55 huku wakibakisha Mechi 2 kumaliza Ligi na kufuatiwa na waliokuwa Mabingwa Azam FC ambao wana Pointi 45 na wamebakisha Mechi 3.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Zacharia Jacob wa Pwani aliyesaidiwa na Hassan Zani na Abdallah Uhako wote wa Arusha, hadi mapumziko Yanga SC walikuwa mbele kwa bao 1-0.

Bao zuri lilifungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Amissi Tambwe dakika ya 40 akimalizia krosi ya winga Simon Msuva.  Dakika nane baada ya kuanza kipindi cha pili, Mrundi huyo aliifungia
Yanga SC bao la pili akiuwahi mpira uliotemwa na kipa Abdul Ibadi kufuatia krosi ya Msuva.

Mfungaji huyo bora wa Ligi Kuu msimu uliopita akiwa na Simba SC, Tambwe akakamilisha hat-trick yake dakika ya 59 akiunganisha vizuri krosi ya Mrisho Ngassa- hilo likiwa bao lake la 14 msimu huu.

‘Golden Boy’, Mrisho Khalfan Ngassa akamsetia na Msuva kufunga bao la nne la la 17 kwake msimu huu, akiendelea kuongoza mbio za ufungaji bora.
Bantu Admin aliifungia Polisi bao la kufutia machozi dakika ya 83 na Tambwe alikabidhiwa mpira baada ya mechi, hiyo ikiwa hat trick ya pili anafunga msimu huu pekee.

Baada ya mechi shangwe za ubingwa zilianza, mashabiki wa Yanga wakiandama kuanzia Uwanja wa Taifa hadi mitaa mbalimbali, ni nderemo na vifijo tu.
Msimamo-Timu za Juu:
1. Yanga Mechi 24 Pointi 55
2. Azam FC Mechi 23 Pointi 45
3. Simba Mechi 24 Pointi 41
4. Mbeya City Mechi 24 Pointi 31
++++++++++++++++++++++++++++

Ushindi huu wa Yanga umepokewa kwa furaha, nderemo na vifijo toka Nchi nzima ya Tanzania huku Mashabiki wakishangilia Timu hiyo waliyoibatiza 'Timu ya Wananchi.' 
MABINGWA WA TANZANIA 


1965 : Sunderland (Dar es Salaam)
1966 : Sunderland (Dar es Salaam)
1967 : Cosmopolitans (Dar es Salaam)
1968 : Young Africans (Dar es Salaam)
1969 : Young Africans (Dar es Salaam)
1970 : Young Africans (Dar es Salaam)
1971 : Young Africans (Dar es Salaam)
1972 : Young Africans (Dar es Salaam)
1973 : Simba (Dar es Salaam)
1974 : Young Africans (Dar es Salaam)
1975 : Mseto Sports (Dar es Salaam)
1976 : Simba (Dar es Salaam)
1977 : Simba (Dar es Salaam)
1978 : Simba (Dar es Salaam)
1979 : Simba (Dar es Salaam)
1980 : Simba (Dar es Salaam)
1981 : Young Africans (Dar es Salaam)
1982 : Pan African (Dar es Salaam)
1983 : Young Africans (Dar es Salaam)
1984 : KMKM (Zanzibar)
1985 : Maji Maji (Songea)
1986 : Maji Maji (Songea)
1987 : Young Africans (Dar es Salaam)
1988 : Coastal Union (Tanga)
1989 : Malindi (Zanzibar)
1990 : Pamba (Mwanza)
1991 : Young Africans (Dar es Salaam)
1992 : Malindi (Zanzibar)
1993 : Simba (Dar es Salaam)
1994 : Simba (Dar es Salaam)
1995 : Simba (Dar es Salaam)
1996 : Young Africans (Dar es Salaam)
1997 : Young Africans (Dar es Salaam)
1998 : Maji Maji (Songea)
1999 : Prisons (Mbeya)
2000 : Young Africans (Dar es Salaam)
2001 : Simba (Dar es Salaam)
2002 : Simba (Dar es Salaam)
2003 : Hamna Bingwa
2004 : Simba (Dar es Salaam)
2005 : Young Africans (Dar es Salaam)
2006 : Young Africans (Dar es Salaam)
2007 : Simba (Dar es Salaam) 
2007–08 : Young Africans (Dar es Salaam)
2008–09 : Young Africans (Dar es Salaam)
2009–10 : Simba (Dar es Salaam)
2010–11 : Young Africans (Dar es Salaam)
2011–12 : Simba (Dar es Salaam)
2012–13 : Young Africans (Dar es Salaam)
2013–14 : Azam (Dar es Salaam)
2014-15 : Young Africans
Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment