Wanawake
wa Kenya hawataki kuwa na wajukuu mapema.hawataki kuwa mabibi ilhali
watoto wao wa kike wakiwa chini ya umri wa miaka 18.
‘’Hofu yao ,
hasa wamama waishio mjini ni kuwa hivi sasa wanawapa watoto wao wa kike
wenye miaka 12 sindano za uzazi wa mpango wakihofu kuwa mabiti zao
watapata ujauzito na kukatiza masomo.
Hivi sasa wanajaribu kila
njia za uzazi wa mpango ili angalau mabinti wamalize elimu ya
Sekondari’’.Wycliffe Onkendi, Ofisa kutoka Wizara ya Afya ambaye
amefanya kazi eneo la Rift Valley ameeleza.
Kulingana ana gazeti la the Standard
matumizi ya njia za uzazi wa mpango kunamaanisha kuwa wanawake hawa
wamekubali kuwa mabinti zao wanajihusisha na ngono zisizo salama wangali
na umri mdogo.hofu yao hasa imejikita katika madhara ya kupata mimba
zisizopangwa kabla ya kumaliza masomo.
Mary Agak, ni Mama na
mfanyabiashara mjini Kericho anasema’’ binti yangu yuko kidato cha tatu
huwa tunaongelea maswala haya mara chache na wanawake wengine kwenye
chama sioni kama ni makosa.kabla ya kuingia kidato cha tatu nilimpeleka
kuchomwa sindano ambayo ilikaa kwa miezi mitatu mpaka mine ni vijana
wadogo damu inachemka huwezi jua watafanya nini’’.
Chanjo ya kuzuia mimba
Mama mwenye watoto watatu anaongeza ‘’bora nizuie balaa hili kuliko kumshuhudia asimalize shule’’.
Ofisa
mmoja katika Zahanati moja mjini Eldoret Paul Anyango anasema ‘’mabinti
walio Sekondari hufika kwenye kituo hicho cha afya wenyewe kwa ajili ya
kupata vipandikizi au sindano wanapokwenda shuleni’’
Hali hii inafanya watu kujiuliza mabinti hawa hufanya nini zaidi ya masomo wanapokuwa shuleni.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment