Siku 8 zimebaki kufikia kilele cha tuzo za filamu mwaka 2015.
Ikiwa
zimebaki siku chache kufikia kilele cha tuzo za filamu kwa mwaka huu
ambapo Tuzo za Filamu Tanzania (TAFA) zinafanyika kwa mara ya kwanza
nchini Mei 23, 2015 Mwalimu Nyerere International Conference Center
jijini Dar es Salaam.
Haya
ni mapinduzi makubwa katika tasnia ya filamu nchini kwani ni kuonesha
mafanikio. Ni vipengele mbalimbali vilivyopo katika kinyang’anyiro cha
tuzo za filamu mwaka huu 2015. Tuzo hizo ambazo ni kubwa na zenye hadhi
ya juu zimeandaliwa na Shirikisho la Filamu Tanzania na washirika
mbalimbali .
“Kazi
kubwa ya Shirikisho la Filamu Tanzania ni kusaidia kukuza tasnia ya
filamu na kuunga mkono jitihada za wasanii kwa namna mbalimbali. Mbali
na hilo pia ni daraja linalowaunganisha wasanii wa tasnia ya filamu na
Bodi ya Filamu nchini hivyo kurahisisha utendaji wa kazi zao. Ninayo
kamati ya maandalizi iliyo imara na thabiti ambayo imefanya kazi katika
mazingira magumu usiku na mchana kuhakikisha tunapata halfa nzuri na ya
namna yake ambayo haijawahi kutokea”, Alisema Simon Mwakifwamba, Raisi
wa Shirikisho la Filamu Tanzania.
Aliongeza
kwa kusema kuwa tasnia ya filamu nchini bado ina safari ndefu
ukilinganisha na Hollywood ambao wameshapiga hatua kubwa. Tuzo hizi sasa
ni jambo wanapaswa kujivunia kwa wasanii na watengeneza filamu
kujivunia. Imeripotiwa kuwa tasnia ya filamu imechangia kwa kiasi
kikubwa ukuaji wa pato la taifa hili linathibitishwa na taarifa ya
mapato nchini ya hivi karibuni, na hili linadhihirisha kuwa tasnia ya
filamu inafanya kazi kubwa ya kupunguza tatizo la ajira nchini ambalo
limekua ni tatizo kwa vijana wengi hapa nchini.
Mara
baada ya uzinduzi wa tuzo za Filamu mwishoni mwa mwaka 2014
uwasilishwaji wa kazi za filamu ulianza kwa wakati na baadae
zilichaguliwa kwa ustadi mkubwa chache zilizoingia katika kinyang’anyiro
cha tuzo hizi na hatua hiyo ilifanikiwa kikamilifu na baadae kutangaza
washiriki wanaowania tuzo hizi za filamu.
Kuna
filamu 24 ambazo zimeingia katika kinyang’anyiro cha tuzo hizi na kati
ya hizo filamu 12 zitaibuka vinara wa tuzo za Filamu Tanzania 2015.
Majaji nao wamefanya kazi kubwa na wana mchango mkubwa, kwani ushindi wa
tuzo utategemea 70% kutoka kwa majaji na 30% zitakua ni kura za
mashabiki. Majaji wote wanatoka katika Mtandao wa Filamu Afrika
Mashariki ambapo Shirikisho la Filamu Tanzania ni mshirika.
Wanatasnia
wa filamu wanayo furaha kwa Shirikisho la Filamu kupiga hatua kubwa na
hatua walizochukua hata kufanikisha kuwapo kwa tuzo hizi pia
wamewashukuru wanakamati wa maandalizi ya tuzo hizi ambao wengi wao
wamejitolea kuhakikisha tunapata kitu cha kujivunia.
Nae
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tuzo hizo Bi Caroline Gul
alisema, “tunategemea kuwa na hafla nzuri na ya kipekee. Tumepokea
maombi mengi kutoka kwa wanatasnia ya filamu ambao wanataka kuhudhuria
kutoka sehemu mbalimbali za Afrika kuwaunga mkono wenzao.
Mbali
na hilo tumeanda burudani kabambe kwaajili ya siku hiyo. Tunachowaomba
watanzania ni kutuunga mkono kwa kununua tiketi na kuhudhuria kwa wingi
kwani ni kuonesha uzalendo kwa kupenda na kuunga mkono jitihada za kazi
za wasanii wetu”
Pia
alizungumzia swala la udhamini kwa kusema kuwa bado muda upo hivyo
wadhamini wajitokeze kudhamini tuzo hizi kwani bado vitu vingi
vinahitajika kufanyika. Alizishukuru taasisi zilizounga mkono tuzo za
filamu ambao ni TCRA, International Eye Hospital na Foreplan Clinic bila
kusahau EATV & EA Radio, Push Mobile na R&R Associates.
0 comments:
Post a Comment