KITUO CHA KUCHAKATA NA KUZALISHA UMEME KWA NJIA YA GESI CHA KINYEREZI I KINATARAJIWA KUKAMILIKA HIVI KARIBUNI.##

fl1
Meneja Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Simon Jilima  (kulia)  akitoa maelezo kuhusu hali ya maendeleo ya mradi kwa wanajopo la ukaguzi kutoka Ofisi ya Raisi Tume ya Mipango, pichani ni  Bibi. Florence Mwanri (Katikati), Ndg, Robert  Masatu na  Ndg. Aloce Shayo, kwa mfuatano.
fl2
Meneja Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Jilima akimwonyesha Naibu Katibu Mtendaji  Ofisi ya Raisi Tume ya Mipango,  Bibi. Florence Mwanri, eneo likatalojengwa kituo cha Kinyerezi II mara baada ya Kinyerezi I kukamilika.
fl3
Sehemu za mashine za kuzalishia umeme wa gesi ambazo ziko tayari katika kituo cha Kinyerezi.
fl4fl6
Mwonekano wa kituo cha kuzalisha umeme wa gesi Kinyerezi kwa juu.
…………………………………………………………..
Kituo cha kuchakata na kuzalisha umeme kwa njia ya gesi cha Kinyerezi I kimekamilika kwa asilimia 88 na kinatarajiwa kuzalisha umeme kuanzia Septemba mwaka huu.
Hayo yalisemwa na Meneja Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Simon Jilima akiwatembeza katika kituo hicho wanajopo la ukaguzi wa miradi kutoka Ofisi ya Raisi Tume ya Mipango walipotembelea mradi huo.   
“Kazi zinazoendelea kwa sasa ni ufungaji wa mifumo katika mitambo; na njia za kusafirisha umeme msongo wa kV 220 kutoka Kinyerezi hadi Kimara na kV 132 Kinyerezi hadi eneo la viwanda la Gongolamboto, alisema Mhandisi Jilima.
Tayari nguzo za kusafirishia umeme kutoka Kinyerezi mpaka Kimara zimeshasimikwa vivyo hivyo kwa upande wa Gongolamboto.
Naibu Katibu Mtendaji  Ofisi ya Raisi Tume ya Mipango,  Bibi. Florence Mwanri, alisema iwapo mradi huu utakamilika na kuanza kuingiza umeme wake katika gridi ya taifa ni dhahiri kuwa gharama za uendeshaji wa viwanda na uzalishaji wa bidhaa zitashuka, na pia kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje.
“Katika miaka mitano ijayo mpango wetu wa maendeleo umejikita zaidi katika uchumi wa viwanda hivyo ni  vema ujenzi huu ukamilika kwa wakati ili kutoleta changamoto katika utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa mwaka 2016/17-2020/21” alisisitiza Bibi. Mwanri.
Ili kuongeza uzalishaji wa nishati hiyo tayari Tanesco wameshanunua mitambo mingine mine ambayo itazalisha umeme kiasi cha kV 180.
Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment