Mnamo 13 mwezi May jenerali
mmoja wa jeshi alitangaza katika redio ya taifa kwamba rais wa Burundi
amepinduliwa na kwamba serikali ya mpito itabuniwa.Lakini msemaji wa
rais alikana habari hizo akidai kuwa kulikuwa na usaidizi mdogo katika
jeshi kwa mapinduzi kutendeka.
13.30-Raia wamlaki rais Ngozi
Mashahidi wameiambia BBC kwamba
rais Pierre Nkurunziza amerudi kwao huko Ngozi nchini Burundi na
amekuwa akiendeshwa katika gari lilo wazi upande wa juu na kwamba raia
wamemlaki kwa shangwe na vigelegele
Maandamano Burundi
Shirika la habari la AFP
limeripoti kwamba rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amerudi nyumbano
kwao huko Ngozi yapata kilomita 140 kazkazini mwa mji mkuu wa Bujumbura
kulingana na duru ambazo hazikutaka kujulikana zilizo karibu na
kiongozi huyo.''Aliwasili katika eneo la Ngozi siku ya Alhamisi.Ni hapa
ambapo anatarajiwa kulihutubia taifa kuhusu jaribio la mapinduzi
lililofeli'',.AFP lilimnukuu aliyetoa habari hizo.
12.00-Raia watakiwa kuendeleza maandamano
Kiongozi wa kundi la kiraia
linalopinga hatua ya rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu amewataka
raia nchini humo kuendelea na maandamano kulingana na shirika la habari
la AFP.
Vital Nshimiriman amesema kuwa licha ya kundi hilo kupinga
jaribio hilo la mapinduzi,vile raia walivyowashangilia wanajeshi wa
jaribio hilo kulionyesha kwamba kuna hamu kubwa ya mabadiliko.
10.30am-Majenerali waasi kushtakiwa
Nukuu muhimu kutoka kwa Gervais
Abayeho,msemaji wa rais Pierre Nkurunziza akizungumza na kipindi cha
BBC cha Newsday.''Mapinduzi hushirikisha watu wengi Kuna wanajeshi wa
nyadhfa za chini ambao wamesalimu amri na ambao wanawasaidia maafisa wa
poisi na uchunguzi wao,lakini ninaamini watu waliopanga mapinduzi hayo
,wale viongozi hilo ni swala jingine ni lazima washtakiwe.hakuna
mgawanyiko katika jeshi.Iwapo unaweza kuwaangalia wale waliokuwa
wakipanga kutekeleza mapinduzi ni wachache ...kundi dogo la
jeshi'',alisema..
10.00am-Majenerali waasi wakamatwa:

Awali
Jenerali Niyombare alikiambia chombo cha habari cha AFP kwamba yeye na
wafuasi wake watajisalimisha akiongezea kuwa ''natumai hawatatuua''.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amesema kuwa amerudi nchini Burund na kwamba anatarajiwa kulihutubia taifa.
0 comments:
Post a Comment