Golikipa
Petr Cech anaweza kumaliza miaka yake 11 ndani ya klabu ya Chelsea
baada ya kuruhusiwa kufanya mazungumzo na timu inayomtaka.
Wakala ya kipa huyo Viktor Kolar,amethibitisha kuruhusiwa kufanya mazunguzo na timu yoyote inayomuhitaji .
“Nina
thibitisha tumeruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu inayomuhitaji Cech
japo anamkataba unaomalizika mwishoni mwa mwaka”alieeza wakala wa kipa
huyo.
Wiki iliyopita Kocha wa Chelsea Jose Mourinho alisema anamuhitaji kipa huyo kuendelea kuitumika klabu hiyo.
Cech
mwenye miaka 32 alijiunga na Chelsea mwaka 2004 na amecheza michezo 16
katika michuano yote msimu huu, akiwa chaguo la pili mbele ya kipa namba
moja Thibaut Courtois.
0 comments:
Post a Comment