
Nyota wa mchezo wa tenesi dunia Maria Sharapova ametinga hatua ya robo fainali ya michuano ya wazi ya italia Sharapova ametinga hatua hiyo baada ya kupata ushindi wa seti 6-3 6-3 dhidi ya mpinzani wake Bojana Jovanovski Petra
Kvitova raia wa Jamuhuri ya Czech nae ametinga kwenye robo fainali
baada ya kupata ushindi wa seti6-3 6-2 kwa kumfunga Jelena Jankovic.
Simona
Halep wa Romania alimshinda Venus Williams kwa seti 6-2 6-1, huku
katika mchezo uliochukua muda wa saa tatu Carla Suarez Navarro,
alimgaragaza vibaya mpinzani wake Eugenie Bouchard kwa jumla ya seti 6-7
(2-7) 7-5 7-6 (9-7).
Mchezaji namba moja Serena Williams
alijiondoa kwenye mashindano baada ya kuumia kiwiko muda mfupi kabla
kumkabili Christina McHale.
0 comments:
Post a Comment