Rais
mstaafu wa awamu ya tatu Mhe. Benjamin Mkapa akifungua Mkutano wa mwaka
wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi leo jijini Dar es salaam.
Rais
mstaafu wa awamu ya Pili Mhe.Benjamin Mkapa akiwa katika picha ya
pamoja na wajumbe wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB).
Rais
mstaafu,Benjamin Mkapa akiwa katika picha ya pamoja na
wawakilishi/wakandarasi waliofanya vizuri na kupewa zawadi mbalimbali na
vyeti na Bodi ya Wasajili wa Wakandarasi (CRB).
Baadhi ya Wahandisi waliohudhuria mkutano huo wakiapishwa leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wahandisi waliohudhuria mkutano huo wakiapishwa leo jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia masuala mbalimbali.
Baadhi
ya zana na vifaa vya ujenzi wakati wa maonyesho kwenye mkutano wa mwaka
wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya zana na vifaa vya ujenzi wakati wa maonyesho kwenye mkutano wa mwaka
wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya zana na vifaa vya ujenzi wakati wa maonyesho kwenye mkutano wa mwaka
wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi leo jijini Dar es Salaam.Picha/Aron
Msigwa -MAELEZO.
……………………………………………………
Na.Aron Msigwa -MAELEZO.
.Dare es salaam.
.Dare es salaam.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe.Benjamin Mkapa amewataka
Wakandarasi kote nchini kufanya kazi zao kwa weledi na kuzingatia
sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia Sekta ujenzi ili miradi
wanayoisimamia na kuitekeleza iweze kuwa na manufaa kwa taifa.
Mhe.Mkapa ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa
ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB)
uliowawajumuisha pia wadau wa sekta ya Ujenzi kutoka nchini Malawi na
Kenya.
Amesema umakini katika usimamizi wa kazi za wakandarasi na
uwepo wa wataalam waliobobea katika sekta ya ujenzi umechangia kwa kiasi
kikubwa kasi maendeleo inayotokea sasa nchini Tanzania.
Ameeleza kuwa sekta ya ujenzi ndiyo iliyolifikisha taifa hapa
kutokana na mchango wake katika Pato la Taifa unaofikia asilimia 14.1
ikifuatiwa na sekta nyingine na kuongeza kuwa ili nchi iweze kuendelea
lazima wakandarasi wazalendo wajengewe uwezo ili kuhakikisha kuwa fedha
zinazotolewa katika sekta ya ujenzi zinabakia Tanzania na kuwanufaisha
wazawa badala ya wageni.
Amesisitiza kuwa uchumi wa Tanzania lazima ubakie mikononi
mwa watanzania wenyewe na kutoa wito kwa Serikali kuendelea kutoa
kipaumbele kwa wakandarasi wa ndani ili wawe na uwezo wa kujiendeleza na
kujitegemea kwa kutengeneza ajira nyingi zaidi na kuiwezesha Tanzania
kuwa nchi ya kipato cha kati.
Amewataka wakandarasi wa ndani kuendelea kufanya kazi zao kwa
kuzingatia weledi, kuzingatia kanuni na taratibu zinazosimamia sekta
hiyo ili taaluma yao iendelee kuheshimiwa ndani na nje ya nchi huku
akisisitiza umuhimu wa wakandarasi hao na kuungana ili kujenga uwezo wa
kushindana na makampuni mengine kutoka nje.
Kwa upande Waziri wa Ujenzi Mhe.John Magufuri akizungumza
wakati wa mkutano huo amesema kuwa ili taifa liweze kupata maendeleo
endelevu katika sekta ya ujenzi lazima wataalamu wanaohusika na sekta
hiyo wafanye kazi zao kwa kuzingatia kanuni, miiko na sheria
zilizowekwa.
Amesema taaluma ya uhandisi nchini Tanzania imechangia kwa
kiasi kikubwa kuimarisha miundombinu ya barabara,
madaraja,majengo,vivuko mbalimbali na miundombinu mingine muhimu ya
kuwarahisishia wananchi huduma bora ya usafiri.
Aidha, amesema uwepo wa sheria na 15 inayosimamis sekta hiyo
hapa nchini na ongezeko la wakandarasi waliosajiliwa wanaofikia 15,062
kutoka ndani na nje ya nchi, wengi wao wakiwa watanzania linaonyesha
maendeleo makubwa yaliyopigwa na sekta hiyo ikilinganishwa na miaka 15
iliyopita.
Amesema Serikali ya awamu ya nne chini ya uongozi wa Rais
Jakaya Kikwete iko katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi
ikiwemo miradi mikubwa ya barabara za mzunguko katika jiji la Dar es
salaam Barabara, madaraja makubwa, reli na miradi mingine ambayo
itaifungua nchi ya Tanzania kitaifa na kimataifa na kuimarisha sekta
usafirishaiji
Ameongeza kuwa Serikali inaendelea kutoa kipaumbele kwa
Wakandarasi wazalendo kote nchini Ili waendelee kunufaika na zabuni
mbalimbali zinazotangazwa kote nchini kwa asilimia 45 na kuongeza kuwa
malengo yaliyopo ni kufikia ongezeko la asilimia 70 ili uchumi wa sekta
ya ujenzi uendelee kubaki nchini Tanzania.
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi Dkt.Ambwene
Mwakyusa amesema mkutano huo umeandaliwa na Bodi ya Wakandarasi Tanzania
kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Sekta ya ujenzi Chini ya kauli
Mbiu isemayo Changamoto na Mustakabali wa Sekta ya Ujenzi katika
Kutimiza Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025.
Amesema licha ya sekta ya ujenzi nchini Tanzania kuendelea
kupata mafanikio nchini bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali za
kihandisi zikiwemo za mazingira yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia
nchi katika kuathiri ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo madaraja
na barabara ambazo zimekua zikiathoriwa na mvua.
Amesema wakandarasi wanakabiriwa na changamoto mbalimbali
ikiwemo ya ucheleweshwaji wa malipo yao na madeni makubwa wanayoidai
Serikali kutokana na miradi waliyofanya katika maeneo mbalimbali nchini.
Amefafanua kuwa mkutano huo wa mwaka umehudhuriwa na wadau
mbalimbali wa sekta ya ujenzi kutoka ndani na nje ya Tanzania wakiwemo
kutoka Kenya na Malawi pamoja na kampuni mbalimbali zipatazo 95
zinazojihusisha na ujenzi zilizoshiriki kuonesha namna zinavyotekeleza
majukumu yao, kuonesha bidhaa wanazozalisha,vifaa vya ujenzi na mitambo
mbalimbali inayotumika katika ujenzi hapa nchini.
Katika hatua nyingine Bodi ya Usajili wa Wakandarasi
imewaapisha Wahandisi waliohudhuria mkutano huo ili kulinda weledi na
ufanisi wa kazi zao na kuwakumbusha wahandisi hao kutumia utaalam wao
katika kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia viwango ,sheria na
taratibu zilizowekwa.
Aidha Bodi ya Usajili wa Wakandarasi imetoa zawadi mbalimbali
ikiwemo vyeti kama motisha ya kutambua mchango wa makampuni na
wakandarasi wazalendo waliofsnya vizuri katika sekta hiyo nchini
Tanzania kwa kuzingatia vigezo mbalimbali ikiwemo suala la uzingatiaji
wa Afya na usalama mahali pa ujenzi,viwango vya ubora wa ujenzi na vifaa
wanavyotumia katika miradi mbalimbali wanayotekeleza.
0 comments:
Post a Comment