Utafiti
umeonesha kuwa watu wanaofanya mazoezi ya kila mara wanaishi kwa miaka
mitano zaidi ya wale ambao hawafanyi mazoezi yeyote.
Aidha
utafiti huo uliowajumuisha watu waliokomaa umebaini kuwa watu walio na
umri mkubwa wanaishi maisha marefu zaidi pindi wanaoacha kuvuta sigara.
Utafiti
huo wa miaka 11 uliwajumuisha watu wazima 5,700 nchini Norway
ulidhibitisha kuwa watu waliofanya mazoezi kwa takriban saa tatu kwa
juma wanaishi zaidi ya miaka mitano zaidi ya wale ambao hawakufanya
mazoezi yeyote.
Wanasayansi hao wameanzisha kampeini za uhamisisho wa faida za kufanya mazoezi hasa kwa watu wazima.
Utafiti huo wa miaka 11 uliwajumuisha watu wazima 5,700 nchini Norway
Wakiandika katika jarida moja la utabibu wa michezo linalochapishwa nchini Uingereza, wanasayansi hao wanasema kuwa maisha ya
kuketi
bila ya kuwa shughuli yeyote inayochemsha damu mwilini inachangia
pakubwa kuzorota kwa uwezo wa mwili kuhimili dhoruba ya maambukizo
tofauti tofauti haswa mtu anapozeeka.
Chuo kikuu cha Oslo
kilithibitisha kufuatia utafiti huo kuwa hata mtu akifanya mazoezi
mepesi ni kheri kuliko kukosa mazoezi kabisa.
Takwimu za utafiti
zinaonyesha kuwa japo watu wenye umri zaidi ya miaka 65 wakishiriki
mazoezi yeyote kwa dakika 150, hiyo itatosha kumweka katika hali nzuri
ya kiafya.
Watu wanaofanya mazoezi ya kila mara wanaishi
kwa miaka mitano zaidi ya wale ambao hawafanyi mazoezi yeyote
Aidha kwa wale wenye umri kati
ya miaka 68 hadi 77 wanahitaji kufanya mazoezi kwa zaidi ya saa moja
kwa juma ilikupata manufaa yake.
Kwa ujumla asilimia 40% ya
washirika waliofanya mazoezi kwa takriban nusu saa kila siku walikuwa
bado hai katika utafiti huo uliodumu kwa miaka 11.
Ripoti hiyo
iliongezea kusema kuwa hata wale wazee waliokuwa na miaka 73 walipoanza
mazoezi asilimia kubwa ilikuwa hai zaidi ya wenzao ambao hawakufanya
mazoezi yeyote.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment