Ligi Daraja la Pili nchini (SDL) mzunguko wa pili unatarajiwa
kuendelea wikiendi hii kwa michezo 12 kuchezwa katika viwanja mbalimbali
nchini, kwa timu nne za juu kutoka makundi A, B, C na D kusaka kupanda
daraja msimu ujao.
Kundi A, michezo mitatu itachezwa ambapo Green Warriors watacheza
dhidi ya Mvuvuma, Abajalo watawakaribisha Mirambo FC uwanja wa Ali
Hassani Miwnyi Tabora, huku Transit Camp wakicheza dhidi ya Singida
United uwanja wa Kambarage siku ya Jumapili.
Kundi B, Madini FC watakua wenyeji wa Alliance FC uwanja wa Mbulu,
AFC Arusha watacheza dhidi ya Pamba uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini
Arusha siku ya Jumapili, huku Bulyanhulu FC wakiwakaribisha JKT Rwamkoma
siku ya Jumatatu uwanja wa Kambarage Shinyanga.
Kundi C, Leo Ijumaa Cosmopolitan watacheza dhidi ya Kariakoo uwanja
wa Karume, Changanyikeni dhidi ya Mshikamano uwanja wa Karume siku ya
Jumatatu, huku Abajalo wakicheza dhidi ya Villa Squad siku ya Jumanne.
Kundi D, Jumamosi Mbeya Warriors watacheza dhidi ya Sabasaba uwanja
wa Sokoine jijini Mbeya, Mighty Elephant watacheza dhidi ya Mkamba
Rangers siku ya Jumapili uwanja wa Majimaji mjini Songea, huku African
Wanderes wakiwakaribisha Wenda FC uwanja wa Wambi Mafinga siku ya
Jumatatu.
0 comments:
Post a Comment