
Vita ya kuwania kupanda daraja msimu ujao itaendelea wikiendi hii
kwa michezo 12 ya Ligi daraja la kwanza nchini (Startimes League)
kuchezwa katika viwanja mbalimbali kwa makundi A, B, C, kwa kila timu
kusaka pointi tatu muhimu.
Leo Jumamosi uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, wenyeji Polisi Dodoma
watakua wenyeji wa Africa Lyon, Kiluvya United wakiwakaribisha Mji Mkuu
(CDA) katika uwanja wa Mabatini Mlandizi, Polisi Morogoro dhidi ya
Kimondo FC uwanja wa Jamhuri, huku Kurugenzi ikiwakaribisha Burkinafaso
kwenye uwanja wa Wambi mjini Mafinga.
JKT Mlale watawakaribisha Njombe Mji uwanja wa Majimaji mjini Songea,
Panone dhidi ya Mbao FC uwanja wa Ushirikia Moshi, Polisi Mara watakua
wenyeji wa Rhino Rangers uwanja wa Karume mjini Musoma, huku JKT Oljoro
wakiwaribisha JKT Kanembwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Ligi hiyo ya StarTimes itaendelea siku ya Jumapili kwa michezo minne
kuchezwa, Friends Rangers watakua wenyeji wa Ashanti United uwanja wa
Karume, Polisi Dar dhidi ya KMC uwanja wa Mabatini Mlandizi, Lipuli
wakicheza dhidi ya Ruvu Shooting uwanja wa Wambi Mafinga huku Polisi
Tabora wakicheza dhidi ya Geita Gold uwanja wa Ali Hassani Mwinyi mjini
Tabora.
0 comments:
Post a Comment