KUPANDA NA KUSHUKA KWA SIMU ZA NOKIA

Image copyrightGetty
Image captionMji wa Nokia nchini Finland ndiko iligunduliwa simu ya Nokia
Je, unaikumbuka siku za Nokia na enzi zake? Jina Nokia linatokaka na mji mdogo nchini Finland, ambapo simu hiyo iliyokuwa maarufu duniani iligunduliwa.
Kwa sasa kuna ishara ndogo kuwa mji huo mtulivu wakati mmoja uliipa simu jina lake, simu ambayo ilibadili kabisa sekta ya simu mapema miaka ya tisini na kubadilisha kabisa uchumi wa Finland kuufanya kuwa uchumi ulioboreka kwa haraka zaidi duniani.
Wakati ikiwa katika kilele chake kwa mapema miaka ya 2000, Nokia iliuza asilimia 40 ya simu zote duniani ambapo ilitambuliwa na kuwa simu maarufu zaidi duniani.
Image captionSimu za Nokia zilichangia robo ya uchumi wa Finland kati ya mwaka 1998 na 2007
Nchini Finland kwenyewe matokeo yalikuwa hata makubwa. Kulingana na taasisi inayofuatilia uchumi wa Finland ni kuwa simu za Nokia zilichangia robo ya uchumi wa nchi hiyo kati ya mwaka 1998 na 2007.
Wakati wa kilele chake, iliwaajiri zaidi ya watu 4,000.
Lakini kwa ghafla soko la simu za Nokia lilishuka kwa kishindo na mauzo kudorora kabisa hali hiyo iyoathiri pakubwa uchumi wa Finland na pia kusabibisha kuwepo kipindi kigumu na kirefu kwa uchumi wa nchi hiyo.
"Nokia ilikuwa ni uti wa mgongo wa kila kitu hapa, kuanguka kwake ilikuwa ni kama jinamizi kwa taifa la Finland kwa mujibu wa mkurugenzi wa uchumi na maendeleo ya mji wa Tampere, Kari Kankaala, mji ulio umbali kidogo kutoka Nokia.
Nokia iliathiriwa sana na kubadilika kwa teknolojia ya simu.
Ilijipata katika njia panda hasa kutokana na kutokea kwa simu aina ya smartphone, na hasa kuzinduliwa kwa simu ya iPhone na kampuni ya Apple mwaka 2007.
Meneja wa zamani wa utafiti wa ustawi katika Nokia Mika Grundstrom anasema kampuni hiyo kwa kiasi kikubwa ilikabiliwa na kizungumkuti.
"Mambo yalianza kuwa magumu. Hatukujua tulifaa kuangazia nini. Tuangazie urahisi wa kutumia simu, kudumu kwa betri au ukubwa wa simu?," anasema.
"Ukifikiria kuhusu betri, tulikuwa na simu zingedumu na moto wiki nzima. Kisha, una simu hii mpya yenye nguvu sana ambayo unahitaji kuichaji kila siku. Sasa utaitangaza vipi kwa mteja?"
Kampuni ya Nokia ilinunuliwa na kampuni ya Microsoft mwaka 2014.
Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment