YANGA YASUKA MIKAKATI YA KUWAKABILI AL AHLY MECHI YA APRIL

KOCHA MKUU wa Yanga anaetoka Holland, Hans van der Pluijm, amesema wanaanza maandalizi kuikabili Al Ahly ya Misri kwenye Mechi ya Raindi ya Pili ya CAF CHAMPIONZ LIGI.
Yanga imefuzu hatua hiyo wa kuitoa APR ya Rwanda kwa Jumla ya Mabao 3-2 kwa Mechi mbili wakati Al Ahly iliibwaga Libolo ya Angola Jumla ya Bao 2-0 baada kutoka Sare 0-0 huko Angola na wao Juzi kushinda 2-0 kwao Alexandria.
Mara ya mwisho kwa Yanga na Al Ahly kukutana katika michuano hii ilikuwa Msimu wa 2013/14 ambapo Yanga walishinda 1-0 Mjini Dar es Salaam na Al Ahly kushinda 1-0 huko Misri na Al Ahly kusonga baada ya kushinda kwa Mikwaju ya Penati 5-3.
Akiongea maraa baada ya kutoka Sare 1-1 na APR, Pluijm alisema kuwa anaijua Al Ahly ni Timu ngumu na inabidi wajipange ili waitupe nje.
CAF CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Pili
**Mechi kuchezwa Aprili 8-10 na Marudiano Aprili 19-20
AS Vita Club [Congo DR] v Mamelodi Sundowns [South Africa]
Al-Merrikh [Sudan] v ES Sétif [Algeria]  
Wydad Casablanca [Morocco] v TP Mazembe [Congo DR]    
Enyimba [Nigeria] v Étoile du Sahel [Tunisia]   
Stade Malien [Mali] v ZESCO United [Zambia]  
Young Africans [Tanzania] v Al-Ahly [Egypt]    
ASEC Mimosas [Ivory Coast] v Al-Ahli Tripoli [Libya]   
Zamalek [Egypt] v MO Béjaïa [Algeria]  
**Washindi kuingia Hatua ya Makundi, Wanaoshindwa kupelekwa CAF Kombe la Shirikisho kucheza Raundi ya Mchujo
Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment