NDEGE NDEFU ZAIDI DUNIANI KUZINDULIWA

Image captionThe Airlander 10 ina urefu wa mita 92 ikiwa ni mita 18 zaidi ya urefu wa ndege ya kawaida.
Picha mpya za ndege ndefu zaidi duniani zimetolewa kabla ya kuzinduliwa kwa mara ya kwanza.
Ndege hiyo inayojulikana kama (The Airlander 10) ina urefu wa mita 92 ikiwa ni mita 18 zaidi ya urefu wa ndege ya kawaida.
Image captionHaina kelele ikiwa angani wala haitoi hewa chafu.
Kampuni moja ya uingereza imechukua miaka 9 kuijenga ndege hiyo katika kiwanda kikubwa zaidi cha ndege cha Cardington kilicho eneo la Bedfordshire
Itaondolewa kwenye kiwanda hicho kwa mara ya kwanza tangu ujenzi wake ukamilike siku ya Jumatatu.
Image captionAirlander 10 inaweza kusimama eneo moja hewani kwa wiki tatu.
Ndege hiyo iliyogharimu dola milioni 25 kuijenga inaweza kusimama eneo moja hewani kwa wiki tatu na na pia inaweza kuendelea kuruka hata baada ya kutobolewa mashimo kwa njia ya risasi.
Jeshi la Uingereza liliishiwa na pesa za kumaliza ujenzi wake kuitumia kama ndege yao ya ujasusi hali iliyosababisha kampuni ya huduma za ndege ya Uingereza kujitwika jukumu la kuikamilisha.
Wengi wanaamini kuwa ndege hiyo isiyo na kelele ikiwa angani wa isiyotoa hewa chafu inaweza kutumiwa kwa usafiri siku za usoni.
Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment