YANGA LEO DIMBANI SAA KUMI JIONI KATIKA MECHI YA PILI RAUNDI YA MTOANO CAF

MABINGWA wa Tanzania Bara Yanga Leo wanatinga Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kucheza Mechi ya Pili ya Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya CAF CHAMPIONZ LIGI dhidi ya Armee Patriotique Rwandaise FC huku wakiwa kifua mbele kwa kushinda Bao 2-1 kwenye Mechi ya Kwanza.
Katika Mechi ya Kwanza iliyochezwa huko Kigali, Rwanda, Yanga iliitandika APR Bao 2-1 kwa Bao za Juma Abdul na Thaban Kamusoko.
Leo Yanga wanahitaji Sare, ushindi au hata wakifungwa Bao 1 kusonga Raundi ya mwisho ya mtoano ambayo watapambana na Mshindi kati ya Al Ahly ya Egypt na Recreativo de Libolo ya Angola ambazo nazo Leo zinacheza Mechi ya Pili huko Borg El Arab Stadium Mjini Alexandria Nchini Misri baada kutoka 0-0 huko Angola.
Kocha Yanga kutoka Holland, Hans van der Pluijm, amesema amekitayarisha vyema Kikosi chake na watacheza ‘Soka Kamili’, yaani ‘Total Footbal’ kuhakikisha wanapata matokeo mema.
Nae Kocha wa APR, Nizar Khanfir ambae anatokja Tunisia, amesema Timu yake bado ina nafasi kwani kwenye Soka lolote hutokea.       
CAF CHAMPIONS LEAGUE
Raundi ya Mtoano ya Timu 32 – Mechi za Pili
RATIBA/MATOKEO:
**Saa za Bongo.
**Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza
14:30 Cnaps Sports – Madagascar v Wydad Athletic Club – Morocco [1-5]
1600  Vitalo FC – Burundi v Enyimba International FC - Nigeria      
16:00 Young Africans – Tanzania v Armee Patriotique Rwandaise FC – Rwanda [2-1]
17:30 AC Leopards de Dolisie – Congo v Mamelodi Sundowns - South Africa
18:30 ES Sahel – Tunisia v Olympique Club De Khouribga – Morocco [1-1]
19:00 Al Ahly – Egypt v Recreativo de Libolo - Angola [0-0]
21:00 El Merreikh - Sudan v Warri Wolves – Nigeria [1-0]    
18:00 Al Zamalek – Egypt v Union Sportive de Douala - Cameroon
Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment