KING'ORA CHA GARI LA MITSUBISHI OUTLANDER CHADUKULIWA


Image copyrightAFP
Image captionMistubishi Outlander
King'ora cha gari aina ya Mitsubishi Outlander kinaweza kuzimwa kupitia wi-fi yake iliopo ndani,watafiti wamebaini.
Mwanya huo unamaanisha kwamba wezi wanaweza kuingia na kutumia tatizo hilo la usalama wa gari hilo kupata mda wa kuvunja,kuingia na kuliiba gari hilo.
Vilevile mwanya huo unaweza kutumika kufanyia udanganyifu mazingira ya gari hilo na kumaliza nguvu betri yake.
Mitsubishi imewataka watumizi wa magari hayo kuzima mtandao wa gari hilo huku ikiendelea kuchunguza tatizo hilo na mfumo wa gari hilo.
Image copyrightMITSUBISHI
Image captionMitubishi Outlander Hybrid
Mtaalam wa maswala ya kiusalama Ken Munro anasema kuwa uchunguzi ulianza wakati alipokuwa akingojea kuchukua watoto wake kutoka shule na kubaini uingiliaji wa mtandao wa gari hilo katika orodha ya simu yake.
Baadaye alibaini kwamba ni gari la Mitsubishi Outlander ambalo ni la rafikiye ambaye aliomuonyesha programu hiyo na vile inavyoweza kutumika kudhibiti gari hilo.
Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment