Akizungumza na wandishi wa habari Kisiwani Pemba amesema kuwa ili kuepuka unene uliokithiri kila mmoja anawajibu wa kufanya mazoezi walau kwa dakika 30 wa siku pamoja na kujiepusha na vyakula vya mafuta mengi yanayotokana na wanyama .
Amesema kuwa ni vyema wandishi wa habari kuvitumia vyombo vya habari kuielimisha jamii umuhimu wa kufanya mazoezi pamoja na kupenda kutumia vyakula vya mafuta yanayotokana na mimea sambamba na wanyama wanaoishi majini wakiwemo samaki na chaza .
Aidha ameeleza kwamba magonjwa yasiyo ya kuambukiza yamekuwa yakipoteza maisha ya watu wengi duniani kote kutokana na jamii kutozingatia masharti yanayotolewa na wataalamu wa afya ikiwemo sauala la kutumia dawa ipasavyo .
Katika hatua nyingine Omar amewataka wandishi wa habari kuhamasika na kujitokeza kwa ajili ya kuchunguza afya zao pamoja na kuihamasisha jamii kuhudhuria klinki kwa ajili ya matibabu na ushauri juu ya magonjwa hayo .
Nao washiriki wa kikao hicho wameutaka Uongozi wa kitengo hico kuandaa bajeti kwa ajili ya wandishi wa habari kufanya vipindi na makala ambazo zitasaidia kuwaelimisha kuhusiana na umuhimu wa kupima afya pamoja na kufanya mazoezi .
0 comments:
Post a Comment