SERIKALI inatambua na kuthamini
mchango wa sekta ya hifadhi ya jamii nchini hasa katika kusaidia kukuza na
kuimarisha uchumi na kuinua hali za watanzania kwa ujumla hasa wale wanaofikiwa
na huduma hizo.
Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa
Mkoa wa Tanga,Salum Chima wakati akifungua semina ya mfuko wa Pensheni wa PPF
kwa maafisa wa makampuni mbalimbali katika (Kanda ya Kinondoni)mkoa wa Tanga.
Amesema kuwa serikali inatambua kuwa
huduma ya hifadhi ya jamii inawafikia watu wachache sana licha ya umuhimu wake
kwa jamii.
Aidha amesema kuwa kwa kutambua
umuhimu huo serikali imekuwa ikiimarisha sekta hiyo ili iwez kupanua wigo wa
watu wanaonufaika na huduma hiyo kwa kurekebisha sheria na kuweka mazingira
bora kwa watu wote wanaojiunga na mfuko huo.
Alifurahishwa kusikia kuwa mfuko wa
Pensheni wa PPF ambayo ilianzishwa mwaka 1978 kwa ajili ya pensheni za
mashirika ya umma lakini pia kisheria inaweza kusajili hata makampuni
binafsi,taasisi za elimu na vyuo binafsi,taasisi za dini na waliojiajiri
wenyewe ikiwemo walioko kwenye sekta isiyo rasmi.
Amesema kuwa hatua hiyo itawafanya
watanzania wengi zaidi waweze kupata huduma bora za mfuko wa PPF na kuwa na
uhakika ya maisha bora ya sasa nay a baadae kama iliyokuwa kauli mbiu ya PPF.
Kwa upande wake,Meneja wa PPF Kanda
ya Kinondoni,Pwani na Tanga,Zahra Kayugwa amesema kuwa watawapeleka mahakamani
waajiri wote ambao watakuwa hawawasilishi michango ya wafanyakazi wao kwa
wakati.
0 comments:
Post a Comment