COASTAL WAMEANZA KUTEKELEZA MAAGIZO YA TFF WATANO WATEULIWA KUSIMAMIA UCHAGUZI MDOGO ##


KIKAO cha Secretarieti ya Coastal Union kilichoketi jana usiku kimeteua majina ya watu watano watakaosimamia Uchaguzi Mdogo wa Klabu hiyo unatarajiwa kufanyika Novemba 23 mwaka huu ili kuweza kuziba nafasi za uongozi zilizokuwa wazi.

Baada ya majina hayo kuteuliwa yatawasilishwa kwenye shirikisho la soka nchini (TFF) kwa ajili ya taratibu nyingine ikiwa ni pamoja na  kutangaza tarehe ya uchukuaji fomu na urudishaji.

Uchaguzi huo unafanyika ili kuweza kujaza nafasi tatu zilizokuwa wazi ambazo ni Mwenyekiti na Wajumbe wawili wa kamati ya utendaji lengo likiwa kuharakisha maendeleo ya Coastal Union.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kikao hicho,Katibu Mkuu wa Coastal Union,Kassim El Siagi alisema kuwa kamati hiyo  iliyoteuliwa wana uwezo mzuri wa kusimamia chaguzi mbalimbali mkoani hapa.

   “Kimsingi walioteuliwa wana uwezo mzuri lakini lazima majina hayo tuyapelekea TFF kwa ajili ya taratibu nyengine zinazofuata na baadae watae watangaze tarehe ya uchukuaji fomu na urudishwaji fomu tayari kwa ajili ya uchaguzi huo “Alisema El Siagi.

Aliyataja majina yaliyopendekezwa kwenye kikao hicho ambao watakuwa chini ya Mwenyekiti wake Abdallah Yahaya,Katibu Mohamed Awadhi na wajumbe wake watakuwa ni Mtwana Akida Boramini,Ibrahim Khatibu na John Joba.

Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment