![]() |
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame |
Akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba , Kamishna Hamdan amesema kuwa tayari askari wameandaliwa kwa ajili ya kufanya doria sehemu za mijini na vijijini ili kuhakikisha amani inatawala sikukuu hiyo .
Aidha amewataka wazazi kuwalinda watoto wao na matendo hatarishi kwa kutowapa vitu vya thamani na ambavyo vinaweza kusababisha athari kwa maisha yao watoto .
Kamanda Hamdan ambaye amefuatana na Mkuu wa Operetion wa Jeshi hilo Zanzibar Hassan Nasir amewasisitiza wananchi kuitumia falsafa ya Polisi jamii kwa kuhakikisha kwamba matendo ya uhalifu yanadhibitiwa .
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh Omar Khamis Othman amewataka wananchi kujiepusha na matendo maovu ambayo yanaweza kusababisha uvunjifu wa amani .
Sala ya idd kifaita ifanyika katika viwanja vya mpira polisi Konde wakati baraza la Idd litafanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Kiislam Micheweni (CSK) ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar DK Ali Mohammed Shein .
0 comments:
Post a Comment