COASTAL UNION YAANZA KUZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA JKT RUVU ##

TIMU ya Coastal Union imeanza maandalizi kabambe ya kuhakikisha inajipanga vema ili kuhakikisha timu hiyo inapata pointi tatu muhimu kwenye mechi yake ya Ligi kuu dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa Jumamosi wiki hii kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani kutokana  na umahiri wa kikosi cha timu hiyo.

Akizungumza  leo mara baada ya kumalizika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly, Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema mapungufu yaliyojitokeza kwenye mchezo wao dhidi ya Tanzania Prison tayari  Kocha wao mkuu  Mkenya  James Nandwa alikwisha kuyafanyia kazi na sasa kikosi kipo kamili kuwavaa maafande hao.

Amesema kuwa mchezo huo utakuwa ni mzuri kwa sababu tayari,Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mkenya James Nandwa alikwisha fanyia kazi kubwa ya kukiandaa timu hiyo na ataingia kwenye mechi hiyo akiwa na lengo moja la kuhakikisha ushindi unapatikana ili kuweza kusogea kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara.

Hata hivyo amesema hakuna mchezaji hata mmoja ambaye ni majeruhi na kuwataka wapenzi na mashabiki kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kwenye mechi hiyo itakayochezwa  kwenye uwanja wao wa nyumbani.
Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment