
Kwa ujumla vitendo vya uhalifu mkoa wa Tanga vimeonekana kupungua kwa
baadhi ya makosa na mengine kuongezeka kwa kiwango kidogo kwa kipindi cha Januari
hadi Novemba 2014 ikilinganishwa
na kipindi kama hicho mwaka 2013. Huu ni mwendelezo wa kushuka kwa takwimu za
uhalifu katika mkoa wetu tangu mwaka
2006/2007 licha ya kuwepo kwa changamoto kadhaa. Takwimu zilizopo
zinaonyesha kuwa jumla ya matukio yote
ya jinai yaliyo ripotiwa Kuanzia Januari hadi Novemba mwaka 2014 ni 17,297,
ikilinganishwa na matukio 17,747 yaliyoripotiwa kwa kipindi
kama hicho mwaka 2013. Huu ni upungufu wa makosa 450, ikiwa sawa na asilimia 2.53%
Kati ya makosa hayo yaliyoripotiwa Januari hadi Novemba mwaka 2014,
Makosa makubwa yalikuwa 2,056 wakati kwa kipindi kama hicho mwaka
2013 yaliripotiwa makosa makubwa 2,124, huu ukiwa ni upungufu wa makosa
68, ikiwa sawa na asilimia 3.20%
Makosa madogo yaliyoripotiwa kuanzia Januari hadi Novemba mwaka 2014
yalikuwa makosa 15,241 wakati kwa kipindi kama hicho mwaka 2013 yaliripotiwa
makosa
15,623, huu ukiwa ni upungufu wa Makosa 382, ikiwa sawa na asilimia
2.44%
Kwa mujibu wa takwimu hizo kwa makosa yote yaliyoripotiwa, Makosa
dhidi ya Binadamu yaliripotiwa kwa kipindi cha Januari hadi Novemba 2014 ni 7,970
ikilinganishwa na makosa 7,805 katika
kipindi kama hicho mwaka 2013 hili ni ongezeko la makosa 165, hii ikiwa ni
sawa na asilimia 2.11%.
Makosa ya kuwania mali yaliyoripotiwa kwa kipindi cha Januari
hadi Novemba 2014 ni 8,183, ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka
2013 ambapo yaliripotiwa makosa 8,572 , huu ni upungufu wa Makosa
389, hi ni sawa na asilimia 4.53%
Makosa dhidi ya Maadili yaliripotiwa katika kipindi cha Januari
hadi Novemba 2014 ni Makosa 1,144 ikilinganishwa na
kipindi kama hicho mwaka 2013 ambapo yaliripotiwa makosa 1,370, huu ukiwa
ni upungufu wa makosa 226, hii ni sawa na asilimia 16.50%
MAKOSA (KESI) MAKUBWA YALIYORIPOTIWA NA JINSI YALIVYOSHUGHULIKIWA
Jumla ya Kesi kubwa 2056 ziliripotiwa kuanzia Januari
hadi Novemba 2014, ambapo Kesi 1031 zipo chini ya upelelezi, Kesi
35 zilifungwa kwasababu mbalimbali za kiupelelezi, Kesi 825 bado zinaendelea
Mahakamani, Kesi 156 zilipata ushindi Mahakamani na Kesi 09 Zilishindwa kupata
ushindi Mahakamani.
Jumla ya Washtakiwa 1684
walikamatwa kutokana na Makosa hayo makubwa, kati ya hao Wanaume ni 1611 na
Wanawake ni 73.
Makosa makubwa ambayo takwimu zinaonyesha yalipungua kuanzia Januari
hadi Novemba 2014 ni pamoja na:-
Ø Uvunjaji, ambapo kwa Januari hadi Novemba Mwaka 2014
yaliripotiwa makosa 373, ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka
2013 ambapo yaliripotiwa makosa 381, huu ni upungufu makosa
08 sawa na asilimia 2.09%
Ø Unyang’anyi wa kutumia nguvu, ambapo kwa Januari hadi Novemba Mwaka 2014
yaliripotiwa makosa 91, ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka
2013 ambapo yaliripotiwa makosa 99, huu ni upungufu makosa
08 sawa na asilimia 8.08%
Ø Wizi mkubwa ambapo kwa Januari hadi Novemba Mwaka 2014
yaliripotiwa makosa 03, ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka
2013 ambapo yaliripotiwa makosa 22, huu ni upungufu makosa
19 sawa na asilimia 86.36%
Ø Kubaka ambapo kwa Januari hadi Novemba Mwaka 2014
yaliripotiwa makosa 329, ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka
2013 ambapo yaliripotiwa makosa 337, huu ni upungufu makosa
08 sawa na asilimia 2.37%
Makosa makubwa ambayo takwimu zinaonyesha yameongezeka ni
pamoja
Ø Unyang’anyi wa kutumia Silaha ambapo kwa Januari
hadi Novemba Mwaka 2014 yaliripotiwa makosa 18, ikilinganishwa
na kipindi kama hicho mwaka 2013 ambapo yaliripotiwa makosa
10, hii ikiwa ni ongezeko la makosa 08 sawa na asilimia
80%
Ø Wizi
wa Pikipiki ambapo kwa Januari hadi Novemba Mwaka 2014
yaliripotiwa makosa 114, ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka
2013 ambapo yaliripotiwa makosa 71, hii ikiwa ni ongezeko la makosa
43 sawa na asilimia 60%
Ø Wizi wa Mifugo ambapo kwa Januari hadi Novemba
Mwaka 2014 yaliripotiwa makosa 364, ikilinganishwa na
kipindi kama hicho mwaka 2013 ambapo yaliripotiwa makosa 341, hii ikiwa ni
ongezeko la makosa 23 sawa na asilimia 6.74%
Ø Mauaji ambapo kwa Januari hadi Novemba Mwaka 2014
yaliripotiwa makosa 100, ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka
2013 ambapo yaliripotiwa makosa 85, hii ikiwa ni ongezeko la makosa
15 sawa na asilimia 17.64%
Sababu ya kuongezeka kwa makosa haya
ni:-
Ø Kuongezeka kwa shughuli za Kiuchumi/
Maendeleo katika maeneo mbalimbali na hasa maeneo ambayo huduma za kiusalama
bado ziko mbali hivyo kuongeza vivutio vya uhalifu hasa wa kutumia Silaha.
Ø Mauaji mengi yaliyojitokeza ni kwa
sababu ya Wananchi kujichukulia sheria mikononi, na wivu wa Kimapenzi.
Ø Aidha kwa upande wa Pikipiki,
kunasababishwa kuongezeka kwa idadi na watumiaji kutochukua hatua za tahadhari za
kiulinzi kwa mali zao hizo, jambo linalopelekea kutengeneza mianya inayotumiwa
na wezi kuiba Pikipiki.
HALI YA MWENENDO WA AJALI ZA BARABARANI
Mchanganuo wa takwimu za
makosa ya usalama barabarani, mwenendo wa takwimu hizi unaonyesha kuongezeka
kwa matukio ya ajali na kupungua kwa matukio ya ajali za vifo.
Mchanganuo wa Matukio ya ajali za
Barabarani
Kwa kipindi cha Januari hadi Disemba 26/2014,
yaliripotiwa matukio ya ajali za Barabarani 102 ikilinganishwa na matukio 96 yaliyoripotiwa katika kipindi kama
hicho 2013 ikiwa ni ongezeko la matukio 06, hii ni sawa na asilimia
6.25%
Ajali za vifo
Kwa kipindi cha Januari hadi Disemba 26/2014,
yaliripotiwa matukio ya ajali zilizosababisha vifo 83 ikilinganishwa na matukio 84 yaliyoripotiwa katika kipindi kama
hicho 2013 ikiwa ni upungufu wa tukio 01, hii ni sawa na asilimia
1.20%
Idadi ya Vifo
Katika kipindi cha Januari hadi Disemba 26/2014, jumla
ya idadi ya watu 116 walikufa kutokana na ajali za barabarani,
ikilinganishwa na watu 129 waliokufa kwa
kipindi kama hicho mwaka 2013. Huu ni upungufu wa idadi ya watu 13, Sawa na asilimia
10.08%
Idadi ya Majeruhi
Katika kipindi cha Januari hadi Disemba 26/2014, Idadi
ya watu waliojeruhiwa kutokana na ajali za Barabarani ni 144 ikilinganishwa na majeruhi
219 kwa kipindi kama hicho mwaka 2013, hii ikiwa ni upungufu wa
majeruhi
75, sawa na asilimia 34.25%
Magari yaliyohusika kwenye ajali hizo ni 152 kwa mchanganuo
ufuatao:-
Ø Magari Binafsi - 29
Ø Mabasi - 24
Ø Malori - 33
Ø Pick up - 07
Ø Pikipiki -
48
Ø Baiskeli -
11
Jumla ya Makusanyo yote yanayotokana
na Notification kuanzia Januari
hadi Disemba 26/2014 ni Tshs.1,054,740,000/= ukilinganisha na muda kama
huo mwaka
2013 ambapo makusanyo yote yalikuwa Tshs. 801,846,000/= hili
likiwa ni ongezeko la Tshs 252,894,000/= sawa na asilimia
32%
Magari yaliyokaguliwa kwa Kipindi cha Januari
hadi 26/2014 ni Magari 16,143
USHIRIKI WA POLISI
JAMII KATIKA ULINZI NA USALAMA
Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga
kupitia kitengo cha Polisi jamii kwa kushirikiana na Wakaguzi tarafa na Polisi
Kata tumefanikiwa kutengeneza mahusiano
/ ushirikiano mzuri na wadau mbalimbali kutoka kwenye jamii inayotuzunguuka
kama vile wafanyabiashara wakubwa na wadogo, viongozi wa ngazi mbalimbali za
serikali, wabunge, madiwani, viongozi wa madhehebu ya dini na wananchi kwa ujumla.
Uhusiano huu unatusaidia kuratibu
ushiriki wa wananchi katika swala zima la ulinzi na usalama katika himaya zao
kwa kuhimiza kuanzishwa kwa kamati za ulinzi na usalama kwenye makundi ya
kijamii, kwa mfano kwenye Nyumba za ibada, maeneo ya biashara, maeneo ya makazi
ya watu na Vikundi vya ulinzi shirikishi.
Mchanganuo wa Kamati za ulinzi na
vikundi vya ulinzi kwenye makundi mbalimbali ya jamii ni kama inavyoonekana
kwenye Jedwali;
JEDWALI LIKIONYESHA IDADI YA KAMATI ZA ULINZI NA USALAMA NA VIKUNDI VYA
ULINZI SHIRIKISHI KWENYE MAENEO YA
MAKUNDI YA KIJAMII -KIWILAYA.
WILAYA
|
KAMATI ZA ULINZI KWENYE NYUMBA ZA
IBADA
|
KAMATI ZA ULINZI KWENYE MAENEO YA
BIASHARA
|
VIKUNDI ULINZI KWEYE NYUMBA ZA IBADA
|
VIKUNDI VYA ULINZI KWENYE MAENEO YA BIASHARA
|
VIKUNDI VYAULINZI KWENYE MAKAZI
|
TANGA
|
05
|
01
|
05
|
01
|
08
|
MKINGA
|
02
|
06
|
02
|
06
|
10
|
PANGANI
|
03
|
12
|
02
|
02
|
12
|
KILINDI
|
03
|
02
|
-
|
-
|
07
|
KOROGWE
|
14
|
08
|
07
|
11
|
97
|
MUHEZA
|
50
|
06
|
12
|
07
|
46
|
HANDENI
|
04
|
04
|
-
|
03
|
06
|
LUSHOTO
|
08
|
28
|
08
|
21
|
157
|
JUMLA
|
89
|
67
|
36
|
51
|
338
|
Aidha elimu ya ukamataji salama,
namna ya kufanya doria, utoaji wa taarifa, namna ya kushuku na haki za wale
wanao washuku na kuweza kuwa kamata na mipaka yao kiutendaji imeendelea
kutolewa kwa Askari wa Vikundi vya ulinzi shirikishi kwa Wilaya zote nane za
Mkoa wa Tanga, ambapo Jumla ya Askari wa Vikundi vya ulizi shirikishi 400
walipatiwa mafunzo hayo na kati ya hao Askari 250 walipatiwa vyeti huko Wilaya
ya Kilindi na wengine waliobakia mpango unaendelea wa kuwapatia vyeti.
Elimu ya ulinzi kwenye malindo
imetolewa kwa Askari wa Makampuni ya Ulinzi yaliyoko Jiji la Tanga ambapo Jumla
ya Askari 40 walipatiwa mafunzo ya Ukakamavu na ulinzi wa kwenye malindo.
Katika kutekeleza mwongozo wa
kusogeza huduma za Kipolisi karibu na Wananchi, Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga
tayari tumeunda Vikosi kazi vya Kipolisi katika Tarafa zote 37 zilizoko Mkoa
wetu wa Tanga.
Kupitia Mfuko wa Wafanyabiashara
dhidi ya uhalifu Mkoa wa Tanga (Tanga Region Business Fund Against Crime) kwenye
Kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa New kwetu Hotel kulipangwa mkakati wa
kuiboresha Karakana ya Polisi iliyoko Kambi ya Polisi Mabawa, kununua Pikipiki
za doria za Polisi, kuendelea kuwapatia posho ya kujikimu kwa Mgambo 20
wanaofanya kazi katika Vituo vidogo vya Polisi.
MATISHIO YA USALAMA
MKOA WA TANGA
Mkoa wetu wa Tanga unazo changamoto
za Matishio ya Kiusalama ambazo zinatokana na mazingira ya Kijiografia, Kijamii, Kiuchumi, na
Kiutamaduni, changamoto hizo ni pamoja na;
Ø Matishio ya Uhalifu wa Kimataifa kama
vile Usafirishaji haramu wa Binadamu, Usafirishaji na matumizi ya Madawa ya
kulevya ya Viwandani na Mashambani pamoja na matishio ya Ugaidi.
Ø Migogoro ya ya Kijamii kama vile,
·
Migogoro ya Ardhi kati ya Wakulima na Wafugaji hasa kwenye Wilaya za Kilindi,
Korogwe, Handeni, Pangani na kwa kiwango kidogo maeneo ya Mkinga.
·
Migogoro ya ardhi kati ya Wawekezaji wa
Mashambani na Wenyeji wanaozunguka maeneo hayo, kwenye Wilaya za
Muheza, Lushoto, Korogwe
·
Mgogoro wa Ardhi kati ya Wachimbaji wadogo wa Madini na Makampuni
yaliyomilikishwa maeneo hayo kisheria. Wilaya za Handeni, Korogwe na Muheza.
Ø Uharibifu wa Mazingira kwa ukataji miti hovyo
hasa eneo la Mwakijembe Wilaya Mkinga na uvuvi Haramu.
Ø Changamoto za upana wa Mpaka kuweza
kudhibiti na kuzuia uhalifu unaovuka mpaka kwani zipo Bandari Bubu zaidi ya
hamsini na njia nyingi zisizo rasmi (Panya
road) hivyo kupelekea changamoto kubwa sana kiusalama.
MIKAKATI YA KUKABILIANA NA UHALIFU KWA MWAKA 2015
Katika kupambana na
Uhalifu, Migogoro mbalimbali na Majanga, tumejiwekea utaratibu kama ifuatavyo;
ü Kuishirikisha Jamii katika kuzuia na
kupambana na uhalifu kwa kutumia Viongozi wa Serikali za Mitaa na Vijiji
kusimamia mpango wa ulinzi shirikishi kwa kutoa taarifa na kuhuisha Vikundi vya
ulinzi shirikishi.
ü Kuhamasisha matumizi ya Daftari la
Makazi ili kubaini Wageni wanaoingia na kuweza kuwafuatilia nyendo zao ikiwa ni
pamoja na sababu za uwepo wao.
ü Kuimarisha usalama kwenye maeneo
ambayo yameonekana kuwa na tatizo kubwa la kiuhalifu kwa kuimarisha doria na
misako ya ghafla.
ü kuwapima madereva wanaoendesha magari
yanayosafiri kwenda nje ya Mkoa wa Tanga kama wana kilevi kila wanapoondoka
Stand Kuu.
ü Kutoa elimu ya matumizi sahihi ya
Barabara kwa wakazi wanaokaa kwenye Vijiji vilivyoko kando kando ya Barabara
Kuu za Mkoa.
ü Kuwasiliana na Maafisa Mifugo ili
kutumia utaratibu wa kutoa vibali kwa mtu anayetaka kuuza au kusafirisha mifugo
yake, hii ikienda sambamba na kuwasiliana na Serikali za Vijiji kulisimamia
vyema zoezi la vibali hivyo, ili
kuwakamata wezi wa mifugo kiurahisi.
ü Kutumia Wakaguzi Tarafa na mfumo wa
Polisi Kata kwa ujumla kama vyanzo muhimu vya taarifa zinazoonyesha dalili za
awali za kuwepo kwa Uhalifu au mgogoro wa makundi fulani ya jamii na
kuyashughulikia mapema kwa kushirikaiana na wadau wengine.
ü Kuendelea kutoa Elimu ya kutosha kwa
askari wetu, hususani katika chumba cha mashitaka kubaini taarifa
zinazopokelewa kituoni ili zile zenye mwelekeo wa migogoro baina ya makundi
fulani ya jamii, zifikishwe kwa viongozi mara moja ili zishughulikiwe haraka.
ü Polisi Mkoa wa Tanga tutahakikisha
kwamba Wananchi wanendelea kupata huduma bora na kwa wakati licha ya kuwepo
changamoto mbalimbali. Pia kwa Askari watakao fanya kazi zao vizuri
watazawadiwa na wale ambao watafanya kazi vibaya na kukiuka maadili ya Polisi
wataadhibiwa ipasavyo kwa mujibu wa Kanuni na Sheria zilizopo. Kwa mwaka 2014
Askari 16 walioadhibiwa kutokana na utovu wa nidhamu na kupewa adhabu
mbalimbali.
ü Kutoa Elimu kwa pande zilizo katika
migogoro juu ya hatua za kisheria zifaazo kuchukuliwa ili kufikia ufumbuzi wa
kudumu wa migogoro husika na kupitia Askari Kata, kuendelea kufuatilia hatua za
utatuzi wa migogoro hiyo katika vyombo husika, ili kuendelea kushauri nini
zaidi chakufanya kama rufaa badala ya kuchukua sheria mkononi.
HITIMISHO
Tunatoa shukrani za dhati
kwa Makundi mbalimbali ya Jamii ya Wakazi wa Mkoa wa Tanga kwa ushirikiano wao mkubwa walioutoa kwa Jeshi
la Polisi na kuendelea kuufanya mkoa wetu kuwa shwari, ni wito kwa Jamii
kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuzuia na kupambana na uhalifu
ili kuleta maendeleo katika mkoa wetu kwani bila usalama hakuna maendeleo.
Tunatoa tahadhali kwa
wale wote ambao wanajihusisha vitendo vya uhalifu waache mara moja kwani
tumejipanga vizuri kwa kushirikiana na Jamii kukabiliana nao, hatutakuwa na
mzaha wala huruma kwa Mhalifu yoyote, wajuwe kwamba siku zao zinahesabika.
Aidha Tunatoa shukrani za Dhati kwa Kamati ya Ulinzi
na Usalama ya Mkoa wa Tanga chini ya Uongozi wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Lt. Chiku Galawa na Mkuu
wa Mkoa wa sasa Mheshimiwa Magalula Said Magalula kwa miongozo na ushirikiano
mkubwa walioutoa kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga kwa kipindi chote cha
kuanzia Januari hadi Disemba 26/2014.
NAWATAKIA HERI YA MWAKA MPYA 2015
WENYE AMANI NA UTULIVU
IMETOLEWA NA (FRASSER KASHAI-SACP)
KAMANDA WA POLISI MKOA WA TANGA
0 comments:
Post a Comment