Klabu 8 toka Nchi 6 ambazo zimetua Robo Fainali ya EUROPA LIGI
zimepatikana Usiku huu baada ya Mechi za Marudiano za Raundi ya Mtoano
ya Timu 16 na England sasa rasmi haina Timu yeyote iliyobakia Mashindano
ya Ulaya baada ya Everton kunyukwa Bao 5-2 na Dynamo Kiev huko Ukraine.
Kupukutika kwa Klabu za England toka Ulaya kunafuatia kutupwa nje kwa
Chelsea, Arsenal na Man City toka UEFA CHAMPIONZ LIGI na kubakiza
natumaini kwa Everton iliyoshinda Mechi ya kwanza kwao Goodison Park 2-1
lakini ikabamizwa vibaya 5-2 na kutupwa kwa jumla ya Bao 6-4.
Droo ya Mechi za Robo Fainali itafanyika Ijumaa Machi 20.
KLABU ZILIZOTINGA ROBO FAINALI:
Club Brugge KV (BEL)
FC Dnipro Dnipropetrovsk (UKR)
FC Dynamo Kyiv (UKR)
ACF Fiorentina (ITA)
SSC Napoli (ITA)
Sevilla FC (ESP)
VfL Wolfsburg (GER)
FC Zenit (RUS)
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment