SERIKALI YAAHIDI KUBORESHA KIWANGO CHA SOKA NCHINI.##

002Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejipanga kufanya Utafiti wa kushuka kwa kiwango cha soka nchini hayo yasemwa Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe.Juma Nkamia,Bungeni Mjini Dodoma tarehe 20.03.2015.

Mhe.Nkamia aliyasema hayo alipokuwa akijibu swali la Mhe.Abdallah Ali Mbunge wa (Kiwani)lililohoji juu ya kushuka kwa kiwango cha soka nchini ikilinganishwa na miaka ya 1970 na 1980,na kusema kushuka kwa soka nchini kunategemeana na vigezo mbalimbali ikiwemo ligi za ndani,Idadi ya Timu zinazoshiriki pamoja na matokeo ya Kimataifa na Viwango vya FIFA.

“Serikali inatoa pongeza Shirika la NSSF pamoja na Timu ya Real Madrid kwa kuanzisha mfumo mzuri wa kuinua soka la Tanzania kwa kuanzisha timu za kuibua vvijana wenye vipaji vya kucheza soka nchini”,alisema Mhe.Nkamia.

Katika kipindi cha maswali ya nyongeza Mhe.Idd Azzan Mbunge wa Ilala, ambaye ni mdau mkubwa wa michezo alihoji juu ya mpango wa Serikali wa kuweka picha za wachezaji maarufu wa zaman katika Uwanja wa Taifa mfano kama mchezaji Abdallah Kibadeni na wengine waliyoiletea sifa kubwa taifa.

Naye Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo alijibu kuwa serikali inashughulikia suala hilo ila kumekuwa na tatizo kubwa la upatikanaji wa picha za wachezaji hao wazamani lakini Wizara itajitahidi kulighulikia hilo kwa ushirikiano na Idara ya Habari Maelezo.

Mbali na hayo Mhe.Nkamia alisema kigezo cha wachezaji wa miaka ya 1970 hadi 1980 kulikuwa na idadi ndogo ya wachezaji ukilinganisha na sasa pia idadi ya klabu za soka zilikuwa hazidi hata 30 kwa wakati huo bali kwa sasa kuna zaidi ya vilabu 100 .

Pia katika miaka ya 1980 Tanzania ilikuwa na wachezaji wasiozidi watano waliokuwa wakicheza soka la kulipwa na kuanzia miaka ya 2000 mpaka sasa kuna wachezaji zaidi ya 15 wanaocheza soka la kulipwa kwa wakati mbalimbali nje ya nchi.
Share on Google Plus

About trustedmishen

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment